Messi: Nina Hamu Kubwa ya Kuendelea Kupambana

Baada ya kibarua cha kutumikia taifa lake kwenye michuano ya kufuzu Kombe la Dunia, Lionel Messi sasa yupo tayari kurejesha majeshi PSG akipania kumaliza mwaka kwa ubora mkubwa.

Messi alikosa mechi mbili za Barcelona kabla ya likizo ya kimataifa, akiwa na shida ya goti na paja, na mpaka sasa bado hajacheka na nyavu kwa mara nyingine akiwa Ligue 1 ambako amecheza mechi tano pekee.

Staa huyu, mshindi wa mara sita wa Ballon d’Or amebainisha kuwa kwa sasa anaendelea vyema na mpango wake ni kuwekeza jitihada kufanya vyema zaidi.

Akizungumzia hali yake amenukuliwa akisema “Naendelea vizuri, vinginevyo nisingecheza”

Lionel Messi

Akizungumzia mpango wake kwa sasa akiwa anarejea kwenye majukumu ya timu PSG, amesema;

“Ni wakati wa kubadilisha zingatio kwa sasa maana bado nina hamu ya kuendelea kupambana kufikia malengo tuliyojiwekea hapa PSG, nahitaji kuwa mzingatiaji na kufanya jitihada kuyafikia”

Messi anatarajiwa kuwepo kweye kikosi cha wikiendi dhidi ya Nantes, Jumamosi, labda ikiwa Pochettino ataamua kumuhifadhi kwa ajili ya kibarua cha Ligi ya Mabingwa waliyonayo Manchester City wiki ijayo.


WIKI NJEMA NA CRAZY TIME CASINO!

Unasababu milioni za kucheza unavyotaka ukiwa na mabingwa meridianbet, lakini unasababu moja ya kushinda mamilioni katika kasino za mtandaoni za meridianbet. Mchezo maridhawa wa Crazy Time unakupa sababu hizo kuwa mmoja wa washindi leo hii.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe