Mwaka jana majira kama haya, ulimwengu wa soka ulikua na habari za kwenda mbele kurudi nyuma. Sakata la Lionel Messi na usajili wa Jadon Sancho, hakika ulitikisa dunia.
Badaa ya kukuru kakara za hapa na pale, dirisha la usajili lilifungwa na hakuna aliyesajiliwa wala kuondoka kwenye klabu yake. Muda hausimami, msimu wa 2020/21 umemalizika na tunarejea sokoni kwa mara nyingine. Safari hii habari ni tofauti. Messi na Sancho, mnatuachaje?

Imeripotiwa kuwa Barcelona ipo mbioni kukamilisha mchakato wa kuongeza mkataba wa La Pulga, baada ya Joan Laporta kushinda uchaguzi mkuu na kuwa raisi mpya wa Barca, aliweka wazi lengo lake la kujaribu kumshawishi Messi kusalia Camp Nou. Inaripotiwa klabu hiyo itafanikisha mchakato huo na kumkabidhi nahodha wako kwenye siku yake ya kuziliwa.
Kule Ujerumani, safari hii Man United hawataki kupoteza muda. Wameanza mapema mchakato wa kujaribu kumsajili Sancho. Borussia Dortmund wamepunguza dau kutoka pauni milioni 108 mpaka milioni 86, kazi kwa United kufanya mambo yawe marahisi.

Licha ya kusambaa taarifa kuwa United walitoa dau la pauni milioni 67 ambalo lilikataliwa, imeripotiwa kuwa safari hii United wametoa dau jipya ambalo kiasi hakijatajwa lakini, inaaminika kuwa Dortmund wanalizingatia dau la sasa na kwamba usajili huu unaweza ukafanyika msimu huu.
Kama taarifa zote mbili nizakuaminika, huenda 2021/22 tutaendelea kumuona Messi akiwa Barcelona na Sancho akiwa katika uzi mwekundu ndani ya Old Trafford kuanzia Agosti 14 vs Leeds United.
SHINDA TSH 150,000,000/=
Mtaani kumechangamka, washkaji wanakamata mkwanja kwa mkakati tu na Footbal Fever! Ni rahisi, changamkia fursa hii kushinda mgao wako wa TSH 150,000,000/= 💰🤑


