Tetesi za Soka Barani Ulaya.

 

Tetesi zinasema, mshambuliaji wa Tottenham na England Harry Kane, 27, amewaeleza wazi wawakilishi wake kwamba atakuwa tayari kuungana tena na Mauricio Pochettino Paris St-Germain.

Arsenal watajaribu tena kusaini mkataba na kiungo wa safu ya mashambulizi wa klabu ya Lyon Ufarnsa Houssem Aouar, 22 na wanajiandaa kumpatia ofa ya mkataba wa malipo ya pauni 100,000 kila wiki.

Tetesi zinasema, PSG watajaribu tena kusaini mkataba na kiungo wa kati wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 28.

 

Tetesi zinasema, mlinzi wa Uskochi Kieran Tierney, 25, amekubali mkataba mpya na Arsenal ambao atausaini katika siku zijazo.

Tetesi zinasema, Sergio Ramos analengwa na Manchester United, PSG na Sevilla baada ya beki huyo mwenye umri wa miaka 35 kuondoka Real Madrid.

Mlinzi wa Real Madrid na France Raphael Varane, 28, bado hajaamua juu ya hatma yake ya baadae, huku kukiwa na taarifa zinazomuhusisha na kuhamia klabu zaa Manchester United na Chelsea.

Tetesi zinasema, Chelsea wameungana na Arsenal katika kinyang’anyiro cha kusaini mkataba na mshambuliaji wa Real Sociedad na Sweden striker Alexander Isak, 21.

Wakala wa Georginho anasema kuwa timu kubwa zaidi za Ulaya zinataka kumsajili kiungo huyo wa kati wa Italia mwenye umri wa miaka 29, lakini huenda asiondoke Chelsea.

Kiungo wa Juventus na Wales Aaron Ramsey, 30, anaweza kurudi Arsenal ambao wanahangaika kuwavutia wachezaji wenye vipaji na wanaweza kumrudia tena mchezaji wao huyo wa zamani.

Tetesi zinasema, Liverpool wana nia ya kumsajili mchezai wa Sassuolo na winga wa Italia Domenico Berardi, 26.

 

Lingard

West Ham watalazimika kumpa kiungo wa kati wa England Jesse Lingard, 28, nyongeza kubwa ya malipo ili kumshawishi asisaini mkataba wa kudumu na Manchester United.

Tetesi zinasema, Watford wanaandaa uhamisho kwa ajili ya mlinzi wa Arsenal Muingereza Ainsley Maitland-Niles, 23.

Arsenal wanajiandaa kutumia karibu pauni milioni 250 katika mikataba mitano mipya ya wachezaji msimu huu, jambo linalompatia fursa Mikel Arteta kujijjenga upya na kufanya mabadiliko katika kikosi chake.

Tetesi zinasema, Wolves wamewasiliana na kiungo wa kati wa Sporting Lisbon 25, Joao Palhinha.


SHINDA TSH 150,000,000/=

Mtaani kumechangamka, washkaji wanakamata mkwanja kwa mkakati tu na Footbal Fever! Ni rahisi, changamkia fursa hii kushinda mgao wako wa TSH 150,000,000/= 💰🤑

Atletico, Atletico Waunga Tela kwa Calhanoglu, MeridianbetINGIA MCHEZONI

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.