Arsenal Wafikia Pazuri Juu ya Kieran Tierney

Kieran Tierney ameripotiwa kufikia hatua kubwa ua mazungumzo na klabu yake ya Arsenal juu ya mkataba mpya wa miaka mitano.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 amecheza mechi 62 na the Gunners tangu alipowasili kutoka Celtic mnamo mwaka 2019 na bado amebakiza miaka mitatu kutekeleza mkataba wake wa sasa kwenye Uwanja wa Emirates.

Tierney alifanikiwa kwa kiasi fulani chini ya Mikel Arteta wakati wa kampeni ya 2020-21, akichangia mabao mawili na kutoa asisti tano katika mechi 38 kwenye mashindano yote.

Arsenal Wafikia Pazuri Juu ya Kieran Tierney

Kwa mujibu wa Telegraph, Arsenal imefikia hatua kubwa ya kukamilisha mazungumzo na mchezaji huyo wa kimataifa wa Scotland kuhusu mkataba mpya wa miaka mitano, ambao utaonyesha umuhimu wake kwa timu hiyo.

Ripoti zinadai kwamba klabu hiyo ya London Kaskazini, ambayo pia inasemekana kuwa katika mazungumzo na Ben White wa Brighton & Hove Albion, wana matumaini ya kumaliza mazungumzo katika siku zijazo.

Tierney, ambaye yupo na kikosi cha Scotland kwenye Mashindano ya EURO msimu huu wa joto, alifunga mara moja na kutoa asisti nne katika mechi 27 za Ligi Kuu msimu uliopita.


SHINDA TSH 150,000,000/=

Mtaani kumechangamka, washkaji wanakamata mkwanja kwa mkakati tu na Footbal Fever! Ni rahisi, changamkia fursa hii kushinda mgao wako wa TSH 150,000,000/= 💰🤑

Atletico, Atletico Waunga Tela kwa Calhanoglu, MeridianbetINGIA MCHEZONI

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.