Chelsea, PSG Vita ya Hakimi Yapamba Moto.

 

Beki wa pembeni wa Inter Milan Achraf Hakimi yuko katikati mwa vita ya uhamisho kati ya Chelsea na Paris St-Germain; Mabingwa wa Serie A wapo tayari kumuuza wangependelea zaidi uhamisho ufanyike kwa wao kupokea pesa taslimu.

Inafahamika kuwa Chelsea wamewasilisha ofa yao ya euro 60m na ​​beki wa pembeni Marcus Alonso anaweza kujumuishwa kama sehemu ya makubaliano hayo.

Inter Milan wanajaribu kushughulikia maswala ya kifedha yaliyowaandama sababu ya janga la coronavirus ambalo limeathiri wamiliki wao wa China, Suning.

Chelsea na PSG pia wametoa ofa yao kwa Hakimi, wakati mchezaji huyo akiwa amekubaliana makubaliano binafsi na miamba hiyo ya Ufaransa.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Morocco alijiunga na Inter msimu uliopita akitokea Real Madrid baada ya kumaliza msimu mzuri kwa mkopo huko Borussia Dortmund kwenye Bundesliga.

Hakimi alikuwa sehemu muhimu ya kikosi cha Inter ambacho kilishinda Serie A kwa mara ya kwanza tangu 2010, akicheza mechi 45 kwenye mashindano yote.


SHINDA TSH 150,000,000/=

Mtaani kumechangamka, washkaji wanakamata mkwanja kwa mkakati tu na Footbal Fever! Ni rahisi, changamkia fursa hii kushinda mgao wako wa TSH 150,000,000/= 💰🤑

Atletico, Atletico Waunga Tela kwa Calhanoglu, MeridianbetINGIA MCHEZONI

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.