Jurgen Klinsmann anasema Tottenham iko moyoni mwake na angependa kuwa bosi wao mpya.
Mchezaji huyo wa zamani wa miaka 56, ambaye amewahi kuwa meneja wa Bayern Munich na Ujerumani, alikuwepo Spurs kwa misimu miwili miaka ya 1990 na bado ni mtu maarufu kwa mashabiki.
Klinsmann alimpigia simu mwenyekiti Daniel Levy wakati Jose Mourinho alipotimuliwa, lakini hakupata majibu, ingawa bado yuko tayari kwa kazi hiyo huko kaskazini mwa London.

Mjerumani huyo alinukuliwa akisema “Nilimpigia baada ya kuachana na Mourinho na kuzungumza naye kuwa ‘Daniel, sasa itakuwaje?”
“Na akaniambia ‘Nina mengi ya kufanya hivi sasa kutatua mambo kwenye kilabu, wacha tuzungumze baadaye baadaye kidogo’. Ndipo nikaona majina yote tofauti yakiingia na kutoka. Iko hivyo hadi leo.
“Spurs iko moyoni mwangu, ningekuwa nao – lakini ikiwa hataki, sitamlazimisha.”
Kazi ya mwisho ya Klinsmann ilikuwa kule Bundesliga na Hertha Berlin lakini aliondoka baada ya miezi mitatu mnamo Februari 2020 na hajafanya kazi ya umeneja tangu wakati huo.
Shughuli ya kumtafuta meneja mpya Spurs imekuwa na mengi tangu walipomfuta kazi Mourinho siku 60 zilizopita, hadi sasa hawajaambulia kitu.
SHINDA TSH 150,000,000/=
Mtaani kumechangamka, washkaji wanakamata mkwanja kwa mkakati tu na Footbal Fever! Ni rahisi, changamkia fursa hii kushinda mgao wako wa TSH 150,000,000/= 💰🤑


