Mike Tyson Alivyomlipia Kisasi Muhammad Alli

October 2 1980, Muhammad Alli anachakazwa vibaya sana na Larry Holmes. Kabla ya pambano madaktari walimkataza Alli kupanda ulingoni kutokana na hali mbaya ya afya yake.

Ila walisahau huyu ni Muhammad Alli, binadamu asiyeamini katika kushindwa na kupoteza. Alilazimisha kupigana akiwa mgonjwa akaambulia kipigo cha ‘mbwa mwizi’

Jukwaani alikuwepo mshikaji wa karibu wa Alli, Cus D’Amato aliyekuja na mvulana mdogo wa miaka 14, Alimuokota katikati ya mji akiwanyang’anya watoto wa kizungu chakula na kuwapiga vibaya.

Tyson na Cus D’Amato

Huyu mtoto aliiabudu mikono ya Muhammad Alli, Aliyahusudu maisha yake na kuuishi unyama wake. Huyu mtoto wa kuitwa Mike Tyson.

Mike Tyson alirudi nyumbani hawezi kuongea, hawezi kula wala kulala. Ilibidi Cus ampigie Alli simu na kumuambia “nipo na kijana fulani hapa, ana ndoto za kuwa Muhammad Alli, tafadhali ongea nae”.

Tyson alishika simu na kuzungumza sentensi moja tu, “Jana nimekutazama ‘live’ kwa mara ya kwanza, usihofu nitakulipia kisasi siku moja.” Ikaisha hivo.

Muda haugandi na jua halikawii kuchwa, Larry Holmes alistaafu ngumi na kurudi nyumbani kupumzika. Tyson alikuja kuitikisa dunia. Holmes akiwa na miaka 38 alitamanishwa kurudi ulingoni kupambana na Tyson kwa kitita cha dola 3 milioni. Tyson alikuwa tayari kupambana bure, pesa si kitu mbele ya kisasi alichokifuga kwa zaidi ya miaka nane.

Pambano likaandaliwa na kupewa jina la ‘Heavy weight history’. Saa hiyo dunia inakumbuka kuwa Holmes hajawahi kupigwa kwa ‘KO’. Muhammad Alli alialikwa kama mgeni wa mpambano.

Kabla ya kengele kulia Muhammad Alli alimfuata Tyson na kumnong’oneza “kumbuka ulichowahi kuniahidi, wakati ni sasa”. Tyson hakumuangusha, ndani ya raundi nne tu Holmes alikula KO ya kwanza ya maisha yake.

Hadithi yangu ya Mike Tyson inaanzia asubuhi moja ndani ya jela ya watoto mjini New York akiwa na miaka 13. Hii ilikuwa mara ya 38 analetwa ndani.

Maafande hapa walimshazoea, ilifika muda wakampa sero yake binafsi yenye jina lake. Si Mapadre wa Roma wala Masheikh wa Saudia waliodhani kama Tyson anaweza kubadilisha tabia..
.
ITAENDELEA..


Ni Muda wa Kuvuna Mkwanja na Jungle Jim and the Lost Sphinx

Hauihitaji kufikira mara mbili ni mchezo gani utakupatia mkwanja ndani ya kasino za Meridianbet. Jiunge sasa ufurahie Jungle Jim and the Lost Sphinx.

  CHEZA HAPA

11 Komentara

    Mike ngumi jiwe

    Jibu

    Tyson yupo vinzur

    Jibu

    Tyson anaeleweka Yuko vizuri

    Jibu

    Kupambana na mtu kama Tyson ni shughuli pevuu.yuko vizuri sana

    Jibu

    Tyson Yuko vizuri

    Jibu

    Nice

    Jibu

    Tyson ni noma

    Jibu

    Nmeipenda hii

    Jibu

    Nice

    Jibu

    Napenda tena tyson arudi ulingoni

    Jibu

    Yupo vizuri tyson

    Jibu

Acha ujumbe