Kuelekea mwishoni mwa kipindi chake, kikosi halisi cha Arsene Wenger, kilijengwa na Mikel Arteta akiwa na Jack Wilshere katika safu ya viungo. Sasa hivi wapo wapi viungo hawa?
Hakika maisha yanakwenda kasi sana. Wakati Arteta akiwa ni kocha wa Arsenal kwa sasa, Wilshere bado anataabika kupata timu ya kuitumikia baada ya kuondoka Bournemouth msimu uliopita.
Wawili hawa (Mikel Arteta na Jack Wilshere) ni maswahiba na waliwahi kuwa mihimili muhimu kwenye kikosi cha Arsenal kwa miaka kadhaa. Maelewano yao ndani na nje ya uwanja, ni sababu ya urafiki wao kudumu kwa miaka mingi.

Imeripotiwa kuwa, Arteta ameiweka milango ya Arsenal wazi kwa Wilshere kujiunga na timu hiyo. Wilshere alikwenda Italia kujiunga na timu ya Como ambayo amekuwa akifanya nayo mazoezi tangu alipoondoka Bournemouth.
Mpaka anaondoka Arsenal, Wilshere alikuwa ameitumikia timu hiyo kwa jumla ya michezo 197 akitwaa vikombe viwili vya FA na alikuwa ni miongoni mwa wachezaji wanaopendwa na mashabiki wa The Gunners.
Akizungumza kuhusu uwezekano wa Wilshere kurejea Arsenal, Mikel Arteta amesema;
Ni mtu ninayemfahamu, nimecheza naye, anapendwa sana kwenye klabu hii na milango yetu ipo wazi.
Arsenal watakua uwanjani wikiendi hii kuchuana na Norwich. Timu zote 2 zimeanza msimu vibaya zikishikilia nafasi 2 za mwisho kwenye msimamo wa EPL.
Meridianbet inakuletea ushindi kwenye kiganjani kwako, unafurahia radha halisi ya burudani ya kasino mtandaoni na tabasamu la ushindi.


