Milovan Rajevac Atimuliwa Timu ya Taifa Ghana.

Shirikisho la Soka Nchini Ghana GFA limemfuta kazi kocha wa timu ya Taifa Milovan Rajevac baada ya kufanya vibaya katika michuano ya AFCON 2021 na kuondolewa katika hatua ya makundi.

 

Milovan Rajevac amedumu kwa miezi mitano tu ndani ya timu hiyo. Taaifa za ndani zinaeleza kuwa kocha huyo hajataka kulipwa chochote baada ya kufutwa kazi hiyo.

Hatua hiyo imekuja baada ya kufanyika kikao kizito baina ya wizara ya michezo na shirikisho la soka la nchi hiyo siku ya jana kufanya tathmini ya kiwango kilichoonyeshwa na Black Stars katika michuano ya AFCON 2021.

Ghana imeshawafuta kazi makocha watatu mpaka sasa chini ya miaka miwili iliyopita:

Januari 2, 2020: Ghana ilimfukuza Kwesi Appiah.

Januari 15, 2020: Ghana ilimteua CK Akunnor na Septemba 13, 2021: Ghana ilimfukuza kazi kocha huyo.

Septemba 20, 2021: Ghana ilimteua Milovan Rajevac leo Januari 22, 2022: Ghana imemfuta kazi Milovan.


JIACHIE NA ALMIGHTY AZTEC

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe