Simba SC Uso kwa Uso na Mtibwa Sugar.

 

Kikosi cha mabingwa watetezi, Simba SC kinavaana uso kwa uso na Mtibwa Sugar leo majira ya saa kumi jioni katika dimba la Manungu, Morogoro katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.

 

Simba SC jana jioni kilifanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Highland kujiandaa na mchezo huo huku wakiwakosa kiungo Jonas Mkude na mshambuliaji Kibu Denis waliopata majeraha katika mchezo wa Mbeya City.

Kocha wa Simba SC Pablo Franco, amesema licha ya Uwanja wa Manungu kutokuwa rafiki sana kwa aina ya soka wanalocheza lakini wamejipanga kucheza kandanda safi la kuwafurahisha mashabiki.

“Jana jioni tumefanya mazoezi ya mwisho kabla ya mchezo wa leo, wachezaji wapo katika hali nzuri. Tunataraji kucheza soka safi ingawa tunajua uwanja hautakuwa rafiki kwetu,” amesema Pablo.


JIACHIE NA ALMIGHTY AZTEC

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe