Tetesi za Soka Barani Ulaya.

Tetesi zinasema, Manchester United imefutilia mbali mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund Erling Braut Haaland baada ya kufahamishwa kuwa mshambuliaji Norway wa miaka 21-angependa kuhamia Real Madrid.

Mshambuliaji wa Uingereza Raheem Sterling, 27, alikuwa tayari kujiunga na Barcelona kwa mkopo kutoka Manchester City kabla ya klabu hiyo ya La Liga kuamua kumsajili winga wa Uhipania wa miaka 21- Ferran Torres.

 

Raheem Sterling

Tetesi zinasema, Mshambuliaji wa Fiorentina Dusan Vlahovic ana ndoto ya kucheza katika Ligi ya Premia, lakini anataka kujiunga na Manchester City badala ya Arsenal.

Mshambuliaji wa Argentina Julian Alvarez anakaribia kujiunga na Manchester City kutoka River Plate kwa mkataba wa miaka mitano, mchezaji huyo wa miaka 21-atasalia Argentina hadi mwezi Juni.

Chelsea, Tottenham na Barcelona wameulizia upatikanaji wa mshambuliaji wa Lille Mcanada Jonathan David, 22, ambaye alifunga mabao12 katika mechi 21 ya Ligue 1 msimu huu.

Tetesi zinasema, Arsenal wanajiandaa kumpatia mkataba mpya wa miaka miwili mkufunzi wao Mikel Arteta, 39, kabla ya mwisho wa msimu ili kuzima nia ya Manchester City kutaka kumchukua.

 

Arteta

Tetesi zinasema, Tottenham wanakaribia kufikia makubaliano na Wolves kumsajili Adama Traore baada ya kuona dau la pauni milioni 15 kwa winga huyo wa Uhispania, 25, lilikataliwa mapema wiki hii.

Beki wa Ujerumani Antonio Rudiger anataka mkataba wa thamani ya £46m kwa ujumla kabla ya kukubali kurerefusha mkataba wake na Chelsea. Mkataba wa beki huyo wa miaka 28 Stamford Bridge unamalizika msimu huu wa joto

Tetesi zinasema, Manchester United wameonesha nia ya kumnunua kiungo wa kati wa Marseille Mfaransa Boubacar Kamara,22, ambaye pia ananyatiwa Roma.



JIACHIE NA ALMIGHTY AZTEC

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe