Mino Raiola: Makubaliano ya Haaland na Real hayajafanyia

Wakala wa Erling Braut Haaland Mino Raiola amekanusha kuwa mshambuliaji huyo wa Borussia Dortmund tayari amekubali kujiunga na Real Madrid msimu ujao wa joto.

Haaland anatazamiwa kuwakutanisha vilabu kadhaa kwenye vita kali ya saini yake huko Ulaya mwishoni mwa msimu huu, dau lake likitajwa kuwa atapatikana kwa pauni milioni 68.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 anasakwa na takribani kila klabu kubwa barani humo, Real Madrid ikiwa ni miungoni akiungana na  Barcelona, ​​Manchester United, Manchester City, Chelsea, Bayern Munich, Juventus, Paris Saint-Germain, na Liverpool.

Mkurugenzi Mtendaji wa Dortmund, Hans-Joachim Watzke alithibitisha wiki hii kwamba Real Madrid wanavutiwa na Haaland, na baadhi ya ripoti zilidai kuwa makubaliano tayari yanaweza kutekelezwa.

Wakala Raiola amekanusha tetesi hizo na kusisitiza kuwa mteja wake atachagua klabu ambayo ni bora kwake, ambayo inaweza pia kumaanisha kusalia Dortmund.

“Haaland anaweza kusubiri timu yeyote. Hatuna makubaliano ya awali na klabu yoyote. Tutatafuta chaguo bora zaidi, na pia sijakataa mwaka mwingine ndani ya Borussia Dortmund.”

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Norway amefunga mabao 19 na asisti 5 katika mechi 16 msimu huu, na ana mabao 76 katika michezo 75 aliyoichezea Dortmund kwa jumla.


Kuwa Bingwa Msimu Huu wa Sikukuu na Ocean Call

Nani hapendi kuwa bingwa na kujishindia mkwanja wa kusahato kuelekea katika sikukuu wiki hii. Mchezo wa Ocean Call kutoka kasino maridhawa za meridianbettz unakupa kila sababu ya kuifanya siku kuu yako kuwa ya kuvutia zaidi.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

Cheza hapa

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.