Mkataba: Mazungumzo ya Depay na Lyon

Mchezaji Memphis Depay na klabu yake ya soka ya Olympique Lyonnais wapo katika muendelezo wa mazungumzo ya kumfanya Mholanzi huyo aongeze mkataba klabuni kwake.

Rais wa klabu hiyo ya ligi kuu ya nchini Ufaransa, Jean-Michel Aulas ameyasema hayo.

Depay alipewa kitambaa cha unahodha kutoka kwa kocha Rudi Garcia kufuatia kuondoka kwa Sylvinho mapema wakati wa msimu wa mwaka 2019-20 na amefunga jumla ya magoli nane kwenye ligi akiwa amecheza mechi 13 pekee kabla hajakumbana na majeraha ya goti kwenye mechi waliyokula kichapo cha 1-0 walipokutana na Rennes mwezi Desemba mwaka jana.

Mchezaji huyo wa zamani wa klabu ya PSV Eindhoven ambaye amekuwa na klabu ya Lyon tangu alipotokea kwa Mashetani Wekundu, Manchester United mwezi Januari mwaka 2017, amesaliwa na mwaka mmoja pekee katika mkataba wake wa sasa dimbani Groupama, lakini OL wanataka waendelee kuwa naye kwa muda mrefu zaidi.

“Lengo lake lilikuwa ni kucheza EURO, ambayo imeahirishwa kwa sasa,| alisema hayo Aulas. Alitaka sana kucheza kwenye hatua ya 16 bora ya michuano ya Champions League katika mechi za pili dhidi ya klabu ya soka ya Italia, Juventus, ambayo ilihairishwa pia pamoja na ile ya fainali ya Coupe de la Ligue BKT. Anajiandaa kuwa tayari kwa hilo.

“Siku zote nimekuwa na mahusiano ya moja kwa moja na mchezaji huyo. Siku zote amekuwa akiniambia kuwa endapo tutakuwa na makubaliano mazuri ya kikazi basi yeye hana shida na suala la kuongeza mkataba wake na atakuwa tayari kufanya hivyo.”

Depay, mwenye umri wa miaka 26, amefunga jumla ya mabao 43 na kusaidia mengine yapatayo 33 katika mechi 102 za Ligue 1 kwa klabu ya soka ya Olympique Lyonnais na amefunga mara sita na kusaidia upatikanaji wa mabao manne kwenye mechi 13 za michuano ya UEFA Champions League kwa klabu hiyo ya Ufaransa.

43 Komentara

    depay ni bonge la mchezaji tatizo anataka kufanya mambo mawili kwa wakati mmoja akeshe studio then asubui aende mazoezini ila kwa vile ligi ya ufaransa ni nyepesi anaweza kuimudu

    Jibu

    Ni vizuri wamuongezee mkataba ili aendelee kubaki hapo

    Jibu

    Gud news kwake,aongeze tu mkataba maana umri wake bado upo fit

    Jibu

    Depay yuko vizuri aongezwe mkataba aendelee kufanya kazi

    Jibu

    Asante meridianbet #kwa taarifa

    Jibu

    Anastahili kuongezewa mkataba ana rekodi nzur

    Jibu

    Ni mchezaji mzuri lakini ni ngumu kufanya vitu viwili kwa wakati mmoja aache tamaa

    Jibu

    Depay mchezaji mahiri sana tatizo hawezi kufanya mambo mawili kwa wakati mmoja…

    Jibu

    Depay ni mchezaji mzuri

    Jibu

    Ni mchezaji mzuri lakini anataka mambo mengi kwa wakati mmoja

    Jibu

    depay amefunga magoli zaidi ya nane kwenye ligi akiwa amecheza mechi 13 so ni mchezaji mzuri

    Jibu

    Depay nimchezaji mahiri

    Jibu

    Lengo lake lilikuwa ni kucheza EURO, ambayo imeahirishwa kwa sasa#meridianbettz

    Jibu

    tatizo anataka kufanya mambo mawili kwa wakati mmoja akeshe studio then asubui aende mazoezini ila kwa vile ligi ya ufaransa ni nyepesi anaweza

    Jibu

    Depay Ni mchezaji mzuri asiependa makuu

    Jibu

    Olympique wanampenda sana Depay#Meridianbettz

    Jibu

    best prayer ever

    Jibu

    Depay ni mchezaji mzuri Sana

    Jibu

    Lyon wana kila sababu ya kumbakisha huyu Depay maana kadhiririsha kiwango chake

    Jibu

    Delay ni mchezaji mzuri tatizo Sasa hawezi fanya Mambo mawili kwa wakati mmoja.

    Jibu

    Kwa kiwango chake Lyon timu inayomfaaa aendelee kukipiga pale

    Jibu

    Katisha kijana Depay yuko vizuri mno

    Jibu

    Depay fundi wa Mpira ..Kama ataongezA mkataba atakuwa amefanya wazo zuri sana

    Jibu

    Depay mchezaj mzur wa muongezeh mkataba tu

    Jibu

    mshika mawili moja mponyoka

    Jibu

    Depay fundi sanaaaa

    Jibu

    wampe mkataba fundi bishoo

    Jibu

    Kwa upande wng inabid aangalie msalai kabla ya mkataba

    Jibu

    Depay kwa Sasa yuko kwenye form

    Jibu

    Depay yuko vizur sana

    Jibu

    Depay yupo vzr sana wamwongeze Mkataba tu

    Jibu

    depay ni bonge la mchezaji tatizo anataka kufanya mambo mawili kwa wakati mmoja music na mpira atulie asakate kabumbu

    Jibu

    Kulingana na record yake kuwa nzuri anastahili kuongezewa mkataba

    Jibu

    Kama wakimuongezea mkataba watakuwa wamefanya jambo la busara.

    Jibu

    Namkubar Sana Depay

    Jibu

    Itakua poa sana

    Jibu

    Shika mbili moja uponyoka tu

    Jibu

    Yupo vizuri anastahili ilo

    Jibu

    Apewe mkataba tu

    Jibu

    Ana rekodi nzuri sana
    #meridianbettz

    Jibu

    Mbona anafanya vizuri kwa nafasi yake apewe uwo mkataba.

    Jibu

    Depay ninamkubali sanaa#meridianbetz

    Jibu

    Yuko vizuri kija

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.