Mambo yameenda kama yalivyokusudiwa na kufikia kuvuka hata matarajio yale ambayo klabu iliyaweka katika maandalizi ya kuifanya siku ya wazee wa Msimbazi kwenda kama ambavyo kila mpenda burudani alidhamiria kuona. Hii imekuwa heshima nyingine kwa kikosi cha Simba kuweza kuiweka mapema kabisa ligi ikiwa haijaanza.
Kwa hakika imeweza kudhihirika kwamba klabu hiyo ina mashabiki wengi na inapendwa sana kwa yale ambayo inayafanya. Pamoja na kwamba ilikuwa kama sehemu ya burudani lakini pia zilikuwa ni salaam kwa wapinzani wake wote ambao atakutana nao msimu huu kutokana na njaa aliyokuwa nayo katika mafanikio.
Kama ilivyo ada wachezaji walipata nafasi ya kuonesha ufundi wao na kuweza kuibua matumaini mengine ya msimu ujao ambapo wao kama klabu jicho lao kubwa ni kucheza katika michuano ya klabu bingwa Afrika na kuandika historia zaidi ya ile ambayo wameiandika msimu huu ndani ya ligi hiyo.
Kuna nyota ambao kwa hakika walikuwa mwiba sana katika mechi dhidi ya klabu ya Power Dynamos ambao wamekubali kupokea dozi nzuri ya goli 3-1 kutoka kwa wenyeji wao ambao walionekana kutawala kila kona ya uwanjani kuanzia ulinzi, kiungo hadi kushambulia. Ni jambo ambalo limeibua matumaini na shamrashamra zaidi.
Mfungaji bora wa msimu uliopita, Meddie Kagere bado amekuwa hatari zaidi kwenye safu ya ushambuliaji katika timu yake jambo ambalo kila mtu analitamani. Kuondoka kwa pacha wake aliyekuwa hatari katika kufumania nyavu, Okwi kwa sasa ameweza kupata watu wengine ambao wamekuwa mwiba na kuweza kumpikia mipira hatari iliyomfanya kufunga magoli matatu ya mapema kwenye ukurasa wake wa kuelekea msimu mpya.
Historia nyingine iliyovunjwa ni mauzo ya tiketi za mechi kuisha kabisa na hata klabu iliweza kuweka wazi hilo ya kwamba mauzo ya tiketi zote 60,000 ambazo ni idadi kamili ya nafasi ambazo zinapaswa kukaliwa na mashabiki husika. Na hata jezi ziliadimika sokoni kutokana na uhitaji mkubwa uliokuwepo ambapo ilitokea kwamba mashabiki walikuwa wakiisubiri kwa heshima kubwa vazi hilo lenye hadhi ya kimataifa sasa ikuwa ni tofauti kabisa na ule muonekano wa awali katika uundwaji wake.
Kwa sasa burudani ndiyo imeanza na kinachosubiriwa zaidi ni burudani ndani ya ligi. Msimu huu utakuwa na mengi ya kuburudisha ambayo kila mwanasoka kwa hakika atavutiwa nayo kutokana na maandalizi ambayo yamefanywa na kila klabu kuelekea msimu mpya pamoja na kwamba bado taarifa za klabu nyingine kuhusu masuala ya usajili yamebaki kuwa siri ya klabu husika.
Povel
Gud news