Kiungo wa klabu ya Real Madrid Luca Modric amesema anajua klabu ya Liverpool itakua imejiandaa kuhakikisha wanalipa kisasi baada ya kuwafunga katika mchezo wa fainali ya ligi ya mabingwa ulaya msimu uliomalizika.
Klabu ya Real Madrid itasafiri mpaka jijini Liverpool kwajili ya mchezo wa ligi ya mabingw barani ulaya hatua ya 16 bora utakaopigwa katika dimba la Anfield siku ya jumanne, Kiungo Modric anasema watakua tayari kukabiliana na vijogoo hao.Mchezo kati ya Liverpool na klabu ya Real Madrid utabeba hisia tofauti kwani klabu ya Liverpool itahitaji kufuta uteja mbele ya mabingwa hao watetezi barani ulaya, Kwani klabu ya Liverpool imepoteza michezo mitatu kati ya minne ya mwisho waliyokutana na klabu ya Real Madrid.
Modric amesema pia kua mchezo wa Real Madrid dhidi ya Liverpool ni miongoni mwa michezo mikali sana ambayo dunia hua inatazama, Lakini limekua jambo la aibu kuwakutanisha mapema kwenye hatua ya 16 bora kwani ingeweza kua fainali nzuri sana kutazama.Luca Modric amesisitiza mchezo huo utakua na maana kubwa sana kwa vilabu vyote viwili huku klabu ya Liverpool wao wakitaka kulipa kisasi, Lakini Real Madrid kwa upande wao wanataka kuendelea rekodi nzuri dhidi ya klabu ya Liverpool ambayo wamekua nayo hivi karibuni.