Bernard Morrison maarufu kama BM33 leo jioni ametangazwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji kuwa mchezaji huru baada ya kamati kujiridhisha kuwa mkataba wake na Yanga kuwa na mapungufu kadhaa.

Morrison, Morrison ni Huru, Meridianbet

Mwenyekiti wa kamati hiyo Elias Mwanjala amesema kuwa mkataba kati ya Morrison na Yanga ulikuwa na mapungufu ambayo yamefanya mkataba huo usiwe na uhalali, hivyo kamati hiyo imefutilia mbali mkataba wake na Yanga na kumfanya kuwa mchezaji huru. Japo Yanga wana nafasi ya kukata rufaa kutokana na huku hiyo.

Morrison, Morrison ni Huru, Meridianbet

Sambamba na hilo kamati hiyo imepeleke Morrison katika kamati ya Maadili kujadili ni kwanini alisaini klabu ya Simba kabla ya shauri lake kutolewa maamuzi na kamati. Pia kamati imemtaka Morrison kulipa pesa ya usajili USD 25000/= aliyochukua kutoka klabu ya Yanga kwaajili ya kusaini mkataba mpya.


Umekuwa mteja muaminifu wa meridianbet? Basi fahamu kuwa kuna zawadi kibao hadi 5% ya pesa yako inarejeshwa kwako. Kila wiki unaweza kurudishiwa mpaka Tsh 250,000.

Soma zaidi

42 MAONI

  1. Ikiwa alichukua Dola 25,000 na fedha hiyo ikawa ndani ya maelezo ya mkataba ina maana alikuwa na mkataba halali hata kama ulikuwa na mapungufu. Ni full ubabaishaji#meridianbettz

  2. Kuna vitu vingine tunatakiwa kujiuliza na kufikiria alisainije mkataba ambao haukuwa na kigezo kama mchezaji maarafu ambaye ameshasaini mikataba mingi na kuichezea yanga ?. kama kamati kuu ya mchezo wamedhibitisha kuwa kunaujanja ambao umetendeka kwenye mkataba wake na yanga kwanini apelekwe kwenye kamati ya nidhamu au ndio kufunika funika mambo yaende?. Yanga kama hawajamlipa pesa zake kwanini asingeshitaki kuwa hajalipwa au hamna mchezaji ambae hatakiwi kulalamika kuhusu haki yake na yanga ikachukuliwa kisheria tunatakiwa tujiulize sio kuchekelea hili.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa