Wakati michezo mbalimbali ikirejea baada ya kusimama kwa muda kutokana na mlipuko wa Korona. Mashindano ya Fomular One – F1 yameongeza muda kwa timu kujisajili kushiriki.
Tarehe ya mwisho iliyopangwa awali (Agosti 12,2020) kwa timu kuanza kujisajili kushiriki michuano ya dunia – F1 World Championship 2021, imesogezwa mbele kwa siku 6 na sasa, kufikia tarehe Agosti 18 timu zitazopenda kushiriki, zinaweza kuanza usajili huku mwisho wa usajili ukiwa ni Agosti 31.
F1 wamesema ” tumepokea mapendekezo mbalimbali ya kisheria ambayo tumeyazingatia. Hivyo, usajili wa mapema utaanza tarehe 18 Agosti”.

Katika kusherehekea miaka 70 ya Grand Prix, timu ya Ferrari, McLaren na Williams walikuwa tayari kusaini mikataba kwa kipindi cha mwaka 2021-2025 kulingana na makataba wa sasa.
Japokuwa, Mercedes wao wameweka wazi kwamba kwa upande wao, bado kuna vitu wanaona vinahitaji kufanyiwa marekebisho kabla hawajaingia makubaliano mapya.
F1 wamebadisha utaratibu wa utoaji zawadi kwa timu shiriki, lengo likiwa ni kuweka usawa na kupunguza utofauti mkubwa uliokuwepo, kati ya timu kubwa na timu ndogo katika michuano hiyo ambayo ilitengenezwa na Mkurugenzi wa zamani – Bernie Ecclestone katika mkataba wa sasa ambao ulitengenezwa 2011.

Ijumaa wiki iliyopita, Mkurugenzi wa Mercedes – Toto Wolff alisema “kampuni yetu (Mercedes) inashida na vipengele vya sheria, biashara na michezo katika mkataba mpya”. Aliongeza kwa kusema wanaona kama F1 hawapo kubadilisha msimamo wao.
F1 walijibu kwa kusema ” tulishirikisha timu zote kwa uwazi na lengo la kuboresha, tuliafikiana kwamba hakutokuwa na muda wa nyongeza zaidi ya hapa”.

Jumapili Wolff alisema ” wanachokitaka F1 ni kutokusogezwa mbele tena. Wameweka siku ya mwisho na wametuelekeza kuifuata kama ilivyo na kusaini mkataba. Sidhani kama kuna mtu atashindwa kuifuata au kampuni kubwa zinahitaji muda zaidi, hili litakuwa tatizo”.
“Huu ni ushirikiano. Wanahitaji timu, na sisi tunahitaji haki ya biashara iliyo na manufaa bora. Siwezi kusema ni suala la siku moja, mbili au wiki. Ni suala linalohitaji uhakika na utayari wa timu ili mambo yaende vizuri”.
Inasemekana, Wolff anapambania kupata pesa nyingi kutoka kwenye F1 kwa kile anachodai kwamba ni sehemu ya kutambua mchango wa Mercedes katika michuano hiyo.

Katika makubaliano mapya, bonasi kwa timu kubwa yameondolewa. Hapo awali, Ferrari walikuwa wanapokea bonasi ya pauni milioni 84, Mercedes na Red Bull pauni milioni 53, McLaren pauni milioni 23 na Williams pauni milioni 7.7
Katika mfumo mpya Ferrari watapokea pauni milioni 30.7 kwa kukaa kwake kipindi kirefu toka kuanzishwa kwa michuano hiyo mwaka 1950.
Kampuni zote zinazotengeneza injini zitapokea dola za kimarekani milioni 10 kwa mwaka kama sehemu ya kutambua mchango wao.
Umekuwa mteja muaminifu wa meridianbet? Basi fahamu kuwa kuna zawadi kibao hadi 5% ya pesa yako inarejeshwa kwako. Kila wiki unaweza kurudishiwa mpaka Tsh 250,000.


Sabrina
Bora wametoa muda wa watu kujisajiri kwa watu waliosalia kufanya usajiri nawao wasajiliwe.
Omary lukumbi
Hii habar mzur
Hope mwaikuka
Mchezo wang pendwa
Samiah
Nimchezo mzuri sanaa
rama
Maoni:vizuri sana
Sauda
Vizuri sana
Nasra
Naukubali huu mchezo
Ester jackson
Asante kwa habari
Latifa juma mohamed
Ni vema wametoa muda wa watu kujisajilibkwa watu waliosalia kufanya usajili nawao wasajiliwe
Lydia Emmanuel Magoti
Mchezo hunao penda nawatu huu nauwerewa Sana yani
farida ahmadi
Habari njema Sana
neema hassan
Gud newZ
Furahav
Jambo zuri,ili timu ziweze kujipanga.
Sadick
Toto Wolff jina kubwa formula One naamini watafikia makubaliana tuendelee mashindano ya kuvutia. Natutiwa sana kumuona Lewis Hamilton akifanya vitu vyake#meridianbettz
magdalena
mchezo mzuri unaopendwa sana na vijana wengi
Tatu
Hii ni habari mzuriii kwa club vyetu
felister
habari njema
Neema
Huu mchezo mzuri sana