Bila shaka leo nikikuuliza unitajie majina ya mashujaa wa Chelsea utawataja wengi lakini unaweza kulisahau jina la Jesper Gronkjaer!
Ndiyo, Gronkjaer ambaye leo anahusika kwa kiasi kikubwa kwenye makala ya leo.
Inawezekana ukajiuliza kwanini Gronkjaer akawa shujaa? wakati labda hatajwi sana au ata hakuusika kwenye mataji mengi ya Chelsea, yani ata hakuusika kwenye kuifanya Chelsea kuwa klabu ya kwanza jijini London kushinda taji la Klabu bingwa Ulaya, anakuwaje shujaa?

Ushujaa wake unatajwa kuja mwaka 2003 pale kwenye uwanja wa Stamford Bridge ambapo Chelsea haikutakiwa kupoteza mechi ya mwisho ya ligi kuu Uingereza ili ifanikiwe kumaliza ndani ya timu nne za juu na kushiriki michuano ya Klabu bingwa Ulaya kwa msimu ujao wa 2003-2004.
Hii isingekuwa mara ya kwanza kwa Chelsea kufuzu kushiriki michuano hiyo ya Ulaya, lakini inakuwaje ushujaa wake unakuja kwenye mechi hii?
Ipo hivi!
Unaambiwa mchezo huo wa mwisho Chelsea ilitakiwa ihakikishe inapata ushindi ili imalize ndani ya timu nne za juu, na ilikuwa inacheza dhidi ya Liverpool ambayo nayo ilitaka ipate ushindi ili ifuzu kushiriki michuano hiyo ya Ulaya, lakini mchezo ulikuwa wa muhimu zaidi kwa Chelsea kwasababu tajiri wa kirusi, Roman Abramovich alikuwa mguu nje, mguu ndani kwenye kuinunua Chelsea, na inaaminika angekuwa mguu ndani kuinunua kama Chelsea ingefanikiwa kufuzu kushiriki michuano ya Klabu bingwa Ulaya.

Hivyo, Chelsea ilitakiwa ifuzu kushitiki michuano hiyo ya UEFA ili mwekezaji, Roman Abramovich ainunue Chelsea.
Liverpool walikuwa wa kwanza kupata goli, likifungwa na Sami Hyppia lakini baadae beki wa Chelsea raia wa Ufaransa ambaye ni mshindi wa Kombe la Dunia mwaka 1998, Marcel Desailly akasawazisha na kufanya ubao kusomeka 1-1 kabla ya Jasper Gronkjaer kufunga goli la ushindi ambalo liliifanya Chelsea kumaliza msimu wa 2002-2003 ikiwa ndani ya timu nne za juu na kufanikiwa kufuzu kushiriki UEFA kwa msimu ujao.

Ushindi huo ukafuatiwa na biashara rasmi ambapo Abramovich akamwaga kiasi kikubwa cha pesa kuinunua Chelsea.
Goli hilo la Gronkjaer likapachikwa jina la goli la paundi bilioni 1 likimaanisha goli lililoruhusu uwekezaji wa bilioni 1 ndani ya Chelsea.
Umekuwa mteja muaminifu wa meridianbet? Basi fahamu kuwa kuna zawadi kibao hadi 5% ya pesa yako inarejeshwa kwako. Kila wiki unaweza kurudishiwa mpaka Tsh 250,000.


Povel
Nakumbuk goal lake liliingiah kwny magol Bora ya msimu hule congrats legendary wetu
Shafii
Gronkjaer atakumbukwa kwa wana Chelsea kwa kufanya Chelsea ifikie hapa hadi Leo.
Devotha
Wapenzi wa Chelsea hawawezi kumsahau wanamkumbuka
Sabrina
Gronkjaer ni balaa
Gabriel
Gronkjaer bonge la mchezaji anastahil kukumbukwa
Mariam mtandama
Habari njema
Hope mwaikuka
Taarifa iko vzur
Rose kapinga
Akumbukwe kwa mazur yake!!!
Rehema
Namkubali Yuko vizuri
Mwajumah
Wapenzi wa Chelsea hawawezi kumsahau wanamkumbuka#Meridianbettz
Dorophina
Kijana ameifanyia Chelsea mambo mazuri sana hawatoweza kumsahau
Sadick
Kumbe nyuma ya goli lake kulikuwa na uwezekezaji wa mabilioni ya fedha#meridianbettz
Adelta
Gronkjaer atakumbukwa kwa kufikisha Chelsea kuwa imara@meridianbettz
Zeiyana
Hana mchango mkubwa sana kwenye clabu ya Chelsea uwezo wake aliutumia hadi kufikia Chelsea hapa hadi leo
Khadija
wapenzi wa chelsea hawawezi kumsahau#meridianbettz
Fatina mfingi
Habar njema
Njiku
Ipo poa hii
aisha
Huyu jamaa ni balaa zito yuko vizuri sana
Ester jackson
Inafurahisha sana mana palikuwa na mambo muhimu ndani yake
Lydia Emmanuel Magoti
Safii hii
Ernest
Sasa nimeelewa ushijaa wa Jesper Gronkjaer, Nadhani Chelsea watamkumbuka sana huyu jamaa
Salma ngende
Yupo vizuri
Caroline
Amefanya Mambo mengi mazuri
Fatuma kasomo
Habar nzuri
Saupha mohamed
Amefanya mambo mazuri
Furahav
Kumbe kulikua na sujaa hatari sana.
magdalena
gronkjaer alikuwa shujaa kweli pale chelsea kwa magoli yake na watamkumbuka sana
felister
Chelsea hawawezi kumsahau uyu jamaa
Tatu
Hii habari nzuri kwa wapenzi was Chelsea kwani imejiwekea history nzuri
David Pere
Gronkjaer atakumbukwa kwa wana Chelsea kwa kufanya Chelsea ifikie hapa hadi Leo.
warda
Mbona mie hata silijui