Mustafi: Tukisaidiana Tutatatua Matatizo Mengi

Mchezaji Mustafi anaamini kuwa ni muhimu sana kuwa na mtazamo chanya juu ya kila kitu maishani.

Ikiwa ni sehemu ya program ya Mental Heath Awareness Week, mlinzi wa klabu ya Washika Mitutu wa London, Arsenal, Shkodran Mustafi aliongelea suala la utu wema na kuwa na mtazamo mwema juu ya kila jambo maishani.

Mlinzi huyo wa Arsenal alijadili juu ya kuepukana na mawazo mabaya maishani na umuhimu wa kutendeana mema wakati wa janga la Corona.

Program ya Mental Health Awareness Week ilifanyika mnamo tarehe 18 hadi tarehe 24 ya mwezi Mei ambapo wachezaji kadhaa wa klabu za soka za Premier League walielezea afya zao za akili.

Kuendelea kuwa na maono sahihi wakati wa mlipuko wa ugonjwa wa Corona ilikuwa ni jambo gumu sana lakini mwanakabumbu wa Arsenal anaamini kwamba unapoamua kuwa na maono chanya juu ya masuala mbalimbali iansaidia sana kukuokoa na matatizo ambayo huenda yangekupata.

“Madaktari wote wanafanya kazi nzuri sana na sisi kama taifa tunajitahidi kupambana na hali hii ila kitu cha muhimu ni sisi kuwa na maono chanya juu ya kila kitu,” alisema hayo Mustafi.

“Endapo tungeweza kuwa na mtazamo chanya juu ya mambo mbalimbali basi tungepata urahisi sana wa kutatua matatizo yetu ya kila siku na kuwa katika hali nzuri sana maishani hasa kifikra na kiafya. Ila ukishikilia kuangalia tu masuala mabaya na mtazamo mbaya utabakia na huzuni muda wote na kuathiri afya zetu.”

Dhamira ya mwaka huu kwenye Mental Health Awareness Week ni kusisitiza upendo na utu wema miongoni mwetu na mwezi uliopita Mustafi alichangia vyakula kwa watu wapatao 16,000 wakati wa kusherehekea siku ya kuzaliwa huko Islington.

“Kwa kawaida siku ya kukumbuka kuzaliwa unapewa zawadi na unakuwa unazungumziwa wewe siku nzma lakini kwa sababu sikuweza kuwa na familia yangu na marafiki zangu na kila mtu awaye yote, nikawaza na kujiambia kuwa ni muda muafaka wa mimi kutoa badala ya kupokea,” alisema.

“Hasa wakati huu ambapo hali ni mbaya na tunapitia magumu maishani, tunatakiwa kujitahidi kusaidiana kwa hali na mali, kufanya yale tunayotaka kufanyiwa na tutaishinda vita hii pamoja.”

48 Komentara

    Yuko sahihi sikuzote mafanikio yanakuja kwa ushirikiano

    Jibu

    Mustafi katisha sana kwa wazo lake

    Jibu

    Nkweli kabsa yupo sahihi umoja ni nguvu

    Jibu

    Mustafi tokea nimjue leo ndo kaongea point#Meridianbettz

    Jibu

    Mustafi anastahl kuwa mfano wa kuigwa kwa jamii..

    Jibu

    Safi sana mustafi mungu akujalie moyo huo huo

    Jibu

    True 🙊

    Jibu

    Ni jambo zuri alilosema Shkodran Mustafi kuwa na umoja wa kutatua matatizo ni suala la utu wema na mtazamo mwema maishani

    Jibu

    Wakiamua wataweza kutatua matatizo ya lakini wanatakiwa wajipange sanaa

    Jibu

    Kwel kwenye ushirikiano kuna mafanikio

    Jibu

    Hajakosea

    Jibu

    Sawa mustafa kweli umoja ni nguvu

    Jibu

    Hasa wakati huu ambapo hali ni mbaya na tunapitia magumu maishani, tunatakiwa kujitahidi kusaidiana kwa hali na mali, kufanya yale tunayotaka kufanyiwa na tutaishinda vita##meridianbettz

    Jibu

    umuhimu wa kutendeana mema wakati wa janga la Corona.ni mawazo mazur aliyo amua pia ni beki mzuri#meridianbettz

    Jibu

    safi

    Jibu

    Hajakosea kabisa na wazo lake .

    Jibu

    Asanteni kwa habari meridianbet.

    Jibu

    Ni mawazo mazuri..

    Jibu

    Hasa wakati huu ambapo hali ni mbaya na tunapitia magumu maishani, tunatakiwa kujitahidi kusaidiana kwa hali na mali kuepukana na huu ugonjwa wa corona na mambo mengine yaendelee

    Jibu

    Mustafi yupo sahihi umoja n nguvu

    Jibu

    Hajakosea ni wazo zuri

    Jibu

    Mental Health Awareness Week inaonekana ni system nzur sana na alichokiongea mustafi yuko sahihi kabisa

    Jibu

    Mustafi katisha kwawazo lake akilinyingi huyo

    Jibu

    Ni vizuri kufanya kazi kwa pamoja

    Jibu

    Yupo sahh anarudish fadhilah kwa jamiii thanks meridian kwa update

    Jibu

    Ni vizur sana kufanya kazi kwa ushilikiano

    Jibu

    Mustafi ni beki mzuri sana na anafanya maana huo ushauri wake ni mzuri sana

    Jibu

    Kuendelea kuwa na maono sahihi wakati wa mlipuko wa ugonjwa wa Corona ilikuwa ni jambo gumu sana lakini mwanakabumbu wa Arsenal anaamini kwamba unapoamua kuwa na maono chanya juu ya masuala mbalimbali iansaidia sana kukuokoa na matatizo ambayo huenda yangekupata.

    Jibu

    Ni kwel kabisa ushirikiano ni nguvu

    Jibu

    Mustafi ameonyesha mfano wa kuigwa sana hasa wa wachezaji wakongwe kama yeye.

    Jibu

    nothing can beat team work haijalishi mko katika hali gani

    Jibu

    Yuko sahihi kabisa kusaidiana ni jambo jema hasa katika kipindi iki kigumu tupitacho na ili janga la corona

    Jibu

    Yupo sawa! Ni kweli wakiungana kwa pamoja wataweza kutatua changamoto zinazo wakabili

    Jibu

    Yuko sawa anarudisha fadhilah kwa huma

    Jibu

    Niwazo mzur

    Jibu

    mustaphi umeongea maneno mazuri sana endelea kuwa na moyo huo huo

    Jibu

    Niwazo zuri

    Jibu

    Bob Marley alisema mkono unatoa ni bora kuliko unaopokea! Mustafa amenena vema na kutenda sawa na maneno yake#meridianbettz

    Jibu

    Yuko sahihi

    Jibu

    Mashabiki wa arsenal . Mpo!?nanyie toeni mtazamo wenu

    Jibu

    Kutoa ni moyo Wala si utajir pongez kwake

    Jibu

    Mustafi yupo sahihi sana#meridianbettz

    Jibu

    Yuko sahihi

    Jibu

    Kazungumza maneno yenye nguvu na wosia ndani yake

    Jibu

    Busara sana hii

    Jibu

    Nice

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.