Neymar amefikia makubaliano na Paris Saint-Germain juu ya mkataba mpya wa muda mrefu huko Parc des Princes, kwa mujibu wa taarifa.
Fowadi huyo wa Brazil, ambaye alikua mwanasoka ghali zaidi ulimwenguni wakati anajiunga PSG kutoka Barcelona kwa pauni milioni 198 mnamo 2017, alitakiwa kumaliza mkataba mwishoni mwa msimu ujao.
Hata hivyo, Neymar hivi karibuni amekuwa kwenye mazungumzo juu ya masharti mapya ya mkataba wake na kijana huyo wa miaka 28 alisema mwishoni mwa wiki kuwa “anafurahi sana” kuwa mji mkuu wa Ufaransa.

Mwandishi wa habari mwenye makao yake nchini Brazil Marcelo Bechler amedai kuwa mazungumzo hayo sasa yamekamilika, nyota huyo wa zamani wa Barca akisaini kandarasi mpya ya miaka minne.
Tangazo rasmi linatarajiwa kutolewa na PSG baadaye wiki hii.
Mabingwa hao wa Ligue 1 pia wanatarajia kumshunikiza mshambuliaji mwenzake, nyota Kylian Mbappe kuendelea kuwepo zaidi ya mwisho wa msimu ujao.
Neptune’s Richies ni mchezo Unaokupa pesa chap chap huku ukiwa unaburudika kupitia Kasino ya Mtandaoni ndani ya Meridianbet.



Magdalena
PSG wamefanya Jambo la maana sana
Rahma
Safi sana amefanya jambo jema
Venerose
Safi sana kijana
Adelta
Kwa Sasa PSG wako vizuri
Caroline
Safi sanaaa
Dorophina
Habari njema kwa mashabiki wa PSG
Hopemwaikuka
Fresh tu
Sarah
Safi
Amiri Kayera
Anapg pesa tu
Sania
Neymar piga kazi
Lydia Emmanuel Magoti
Safii sana
warda
Jamani mwenyewe alitaka akacheze na Messi