Ni Pesa Nyingi Sana!

United watatakiwa kulipa hela ya kihistoria itakayovunja rekodi nyingi zilizowekwa kama bado wana uhitaji wa kumnasa mlinzi wa timu ya taifa ya Uingereza, Harry Maguire. Hilo linakuja pale ambapo mchezaji huyo amezidi kupanda thamani ndani ya kikosi hicho kwa klabu ya Leicester kuweka dau lao la juu ambalo ni £90m kwa yeyote mwenye mapenzi ya nyota huyo.

Mashetani Wekundu walimhitaji mchezaji huyo hata kabla ya msimu huu na walifikia gharama ya £75m kwa kutaka kukamilisha kabisa usajili wake lakini jambo hilo liligonga mwamba kutokana na klabu inayommiliki mchezaji huyo kusimamia suala la gharama wanayohitaji kumuachia.

Huku kukiwa na ugumu kwa sasa na ubovu wa safu ya ushambuliaji ni hakika kuwa wanahitaji mtu ambaye atakipa nguvu kikosi hicho hasa eneo lao lenye majanga makubwa sana katika kampeni za ubingwa na kuweka mambo sawa wameamua kurudi kumuwinda kwa awamu nyingine lakini ughali wa mchezaji huyo unaibuka na kuwa juu sana.

Baada ya kusajiliwa kutoka Hull mwaka 2017 mlinzi huyo ameongeza upekee zaidi ndani ya kikosi hicho kwa kukipa matokeo hadi kukisimamia kilete ushindani kwa klabu yoyote wanayokutana nayo. Pia, amekiongoza kikosi cha timu ya taifa kwenye michuano ya Euro iliyopita na pia kwenye kombe la dunia.

Katika miaka yake 26 kiwango chake kimeendelea kupanda kwa kasi. Endapo atafanikiwa basi ni hakika atachagiza sana kuifikisha timu hiyo mbali zaidi katika ramani za kimataifa na kwenye mashindano mengine yote ya ndani. Kwa sasa wanachohitaji ni nani wa kusaidiana na Lindelof katika harakati hizo kwa sababu tangu mchezaji huyo asajiliwe 2017 amejaribu kuonesha kitu fulani cha pekee kikosini hapo kinachofanya angalau mapungufu yasionekane yale ambayo yanaoneshwa mara kwa mara na wachezaji anaofanya nao kazi uwanjani.

Endapo biashara hiyo haitapewa nafasi kama matarajio ya klabu hiyo yanavyoonesha basi matajiri hao watarudi nyuma kumuwinda kwa mara nyingine Koulibaly ambaye wamemuwekea kipaumbele katika mipango yao kwa kipindi kirefu. Mchezaji huyo amekuwa na mchango mkubwa sana ndani ya Napoli na hilo linawapa nguvu United.

Ni imani ya kila mmoja kwamba mchezaji hutamani sana kucheza kwenye klabu ambayo inaonesha kutwaa sana mataji na ina malengo makubwa ya muda mrefu. Kwa nafasi hiyo Leicester hawana nafasi kubwa kuendelea kumshawishi sana Maguire asalie. Kama ataamua kutimka hawataweza kumzuia kabisa.

2 Komentara

    Hongera yao

    Jibu

    Habar njema

    Jibu

Acha ujumbe