Nike Wavunja Mkataba na Mason Greenwood

Kampuni kubwa duniani inayotengeneza vifaa vya michezo Nike imesitisha mkataba wake na mchezaji wa kimataifa wa Uingereza anayecheza kwenye klabu ya Manchester United Mason Greenwood.

Mason Greenwood alikamatwa tarehe 30 January na police wa Greater Manchester Police, baada ya aliyekuwa mpenzi wake Mason Greenwood kuchapisha picha kwenye mtandao wa kijamii huku akiandika “haya muone Mason Greenwood anavyonifanyia kwa msiomjua” na  aliwekwa kizuizini kwa siku tatu kabla ya kuachiwa kwa dhamana siku ya jumatano.

NIKE

Siku ya kwanza kukamatwa kwake kutokanana shutuma za unyanyasaji wa kingono, kampuni kubwa ya vifaa vya michezo Nike walisema, “tunafwatilia kwa karibu tuhuma hizo”, Greenwood amekuwa akidhaminiwa na kampuni hiyo tokea mwaka 2019 lakini sasa kampuni hiyo imeamua kuachana nae.

Msemaji wa kampuni ya Nike alinukuliwa kwenye mahojiano na The Athletic, “Mason Greenwood sio tena mwanafamilia ya Nike” kampuni mbalimbali zikiwemo za michezo ya kieletroniki FIFA, eFootball na PES wote wamemuomdoa kwenye michezo yao.

Greenwood ameichezea Manchester United michezo 129 na amefunga magoli 35, japo ametoka kwa dhamana klabu ya Man Utd imesema kuwa haitamruhusu kushiriki mazoezi wala kufanya kazi yeyote ya klabu mpaka pale watakapo toa tamko.


 

KASINO YA MTANDAONI: EMOTICOINS SABABU YA KUVUNA ZAIDI.

Haijawahi kuwa rahisi hivi kwenye safari yako ya kuvuna mkwanja, kasino maridhawa ya meridianbettz inakuletea mchezo wa Emoticoins unaokupa nafasi ya kufanya safari yako kuwa rahisi zaidi. Wakati ni wako nafasi ni yako na Emoticoins.

senegal, Senegal Mabingwa AFCON 2021., Meridianbet

CHEZA HAPA.

Acha ujumbe