"Nime miss Sana Soka" -Jurgen Klopp

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amesema kuwa amemiss sana soka na anatamani kurejea ili aone kikosi chake kikiendelea kufanya makubwa baada ya likizo ya lazima ya Corona.

Klopp anasema atakuwa na furaha isiyo kifani akiwashuhudia Liverpool wakirejea tena dimbani. Kwa sasa klabu za EPL zipo kwenye maandalizi ya kurejea Juni 17.

Liverpool wapo kileleni kwa ponti 25 zaidi, wakiwa wanafukuzia taji lao la kwanza kwa miaka 30 sasa. Bila shaka hii ni nafasi ambayo Liverpool hawahitaji kabisa kuipoteza.

Kulikuwa na wasiwasi ikiwa janga hili la Corona lingekwamisha jitihada walizozionesha Liverpool kutwaa ubingwa kwa namna yeyote. Kuendelea kwa ligi ni tumaini kwao.

Kama ilivyo kwa wapenzi wengine wa soka, wakati huko kimara na mwenge wakisema wana “Mzuka wa kurejea” kwa ligi, Klopp yeye anakwambia “”I have missed it so much it’s unbelievable”, akimaanisha amekumbuka kuwepo dimbani balaa!

Tazama mizuka ya Klopp anapokuwa dimbani, ameikumbuka sana furaha hii 👇

Hata hivyo, Klop amesema bado kuna kazi kubwa sana ya kuifanya wakati Liverpool wakihitaji kushinda mechi nyingi zaidi kadri inavyowezekana ili kujiweka kwenye uhakika zaidi wa kutwaa taji hili msimu huu.

Baada ya kutwaa Ubingwa wa Ulaya mwaka jana, sasa ni wakati wa kutwaa taji la ligi, na kwa mujibu wa meneja huyu ni kuwa hakutakuwa na uafadhali wa nyumbani, mechi zote zitapewa uzito sawa.

EPL imesalia na mechi 92 na mechi zote zinatarajiwa kuwa ziatakuwa zinachezwa bila mashabiki na wachezaji watakiwa kupimwa kila baada ya wiki mbili.

 

48 Komentara

    habari nzuri kwetu sisi mashabiki ata sisi tumekumisi sana kukuona jurgen

    Jibu

    Kweli kila wapenda soka tulimiss kabumbu

    Jibu

    Me naiyombea Liverpool ichukue hata ubingwa kwa mwaka huu.

    Jibu

    Tuliishia vizuri sisi mashabiki Wa Liverpool tunasubiri kwa hamu muendelezo

    Jibu

    Mashabiki wako tumekumisi pia

    Jibu

    anatamani kurejea ili aone kikosi chake kikiendelea kufanya makubwa baada ya likizo ya lazima ya Corona.

    Jibu

    Vile Yuko na hamu sasa na hii ktu

    Jibu

    Ni kweli lazima amiss soka na hata sisi mashabiki pia tumemiss soka ile mbayaaa

    Jibu

    Ni habari nzuri kwetu mashabiki wako tumekumis pia

    Jibu

    Habari mjema

    Jibu

    Wapenzi wa liverpool tunasubr kwa hamu..

    Jibu

    Sio kwa klopp tu kila mdau wa soka ana hamu ya kuona mwendelezo wa ligi mbali mbali

    Jibu

    ameikumbuka mizuka yake pindi anapokua dimbani

    Jibu

    Tulikuwa na wasiwasi ikiwa janga hili la Corona lingekwamisha jitihada walizozionesha Liverpool kutwaa ubingwa kwa namna yeyote. Kuendelea kwa ligi ni tumain la kweli tu

    Jibu

    Nimefurahi kusikia mambo yanarudii siku si nyingi. Tumemic sana

    Jibu

    Sisi mashabiki tumemisi Sana kumwona
    Jurgen klopp akiwa uwanjani

    Jibu

    Tumemisi sana kumuona Klopp

    Jibu

    Makala safi ila wote tupo pamoja jurgen klopp

    Jibu

    Hata mie nimemic kwa Kweli #Meridianbettz

    Jibu

    Nami natamani kuona Liverpool ikichukuwa ubingwa

    Jibu

    Wengi tumemisi soka jamani tunasubir kwa ham sana

    Jibu

    Wote tumemisi soka,ili tushuhudie liver inavyobeba kombe baada ya miaka 30.

    Jibu

    Habar njema

    Jibu

    Epl panapo hali shwari sina shaka na kulibeba Liverpool ….ninachokisubiri kwa hamu ni Kuwaona ELLIOT,WILLSON,Curtis jones,grujic wakipewa nafasi zaidi na kuwa world class players pale Liverpool chini ya KLOPP….YNWA

    Jibu

    Msimu huu inaimani majogoo ya mji yatachukuwa ubingwa

    Jibu

    Klop hana lolote anachekelea ubingwaa tu wa EPL

    Jibu

    Soka ndo linarudi hilo jurgen, soon tu tunaingia uwanjan

    Jibu

    Huyu kocha no chizi wa soka so mchezo Ndio maana anaona Kama ligi inachelewa kurudi

    Jibu

    Safii tulikuwa tunasubili kwahamu Mambo mazuri tumemic Sana nasisi

    Jibu

    Klopp hua ana mizuka sn uwanjan.. namkubal

    Jibu

    Baada ya kutwaa Ubingwa wa Ulaya mwaka jana now ana angalia ubingwa wa epl ili kutoa gundu la mda mrefu

    Jibu

    Tuendelee kuomba.. Mungu atafanya njia

    Jibu

    Amesema Jambo la kweli Liverpool watazidi kufanya mambo makubwa

    Jibu

    Ata Mimi nilimis Sana soka na kumwona klopp.

    Jibu

    Daaah…! Nimic kumuona mo Sarah akiwa dimbani kwa mala yengine tena

    Jibu

    Jurgen klopp kocha anamachachali sana

    Jibu

    Ianze tu wakipgeh tumemic hta mashabiki

    Jibu

    Mashabiki wa Liverpool tunaungana na ww tunasubiria kwa hamu

    Jibu

    Kocha wa soka anatarajia kufanya mambo makubwa sana pale EPL

    Jibu

    Mpira una burdani moja tam Sana na ambayo mtu huwwz kuisahau na matokeo ya kusisimua

    Jibu

    Ianze tuu maana mashabikitumeimis

    Jibu

    Klop anatuzuga tuu anataka ligi irudi ili akabidhiwe kombe lake wafanye sherehe.

    Jibu

    hata sisi tumemiss vituko vyake ila huyu kuna siku atampiga mtu ngumi maana ana mchecheto sana klopp

    Jibu

    Tumemiss vituko vyake klopp
    Liverpool watachukua ubingwa baada ya miaka 30 kupita#meridianbettz

    Jibu

    Kuwa mkwer mzee baba sema tyuu umemiss kunyakua kombe

    Jibu

    Klopp tumekumis hatari hatari kuona bwebwe zake

    Jibu

    Nikweli kabisa tumimic Sana soka

    Jibu

    Tumemic Sana kwakwer

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.