Mshambuliaji wa klabu ya Liverpool Darwin Nunez amekabidhiwa jezi namba tisa ambayo ilikua ikivaliwa na mshambuliaji Roberto Firmino ambaye ametimka klabuni hapo.
Nunez ambaye alisajiliwa kwa gharama kubwa msimu uliomalizika akitokea Benfica ya Ureno aliingia ndani ya Liverpool akakabidhiwa jezi namba 27, Lakini baada ya Firmino kuondoka akakabidhiwa jezi namba 9 ambayo alikua akivaa Benfica.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uruguay amekua na kiwango kizuri katika timu japo hajafikia matarajio ya wengi ambayo wamekua nayo, Lakini hakua kwenye kiwango kibaya na ndio maana ameaminiwa na kupewa jezi hiyo.
Darwin Nunez anaungana na baadhi ya magwiji ambao wamewahi kuvaa jezi namba 9 ndani ya klabu ya Liverpool kama Robbie Fowler, Fernando Torres, pamoja na Roberto Firmino ambaye ndio amemuachia jezi hiyo wote wakiwa wamefanya makubwa kwenye jezi hiyo.
Mshmbaliaji Nunez ana deni kubwa la kulipa kwenye jezi namba 9 ndani ya viunga vya Anfield kwani magwiji waliovaa jezi hiyo wamefanya makubwa hivo na raia huyo wa kimataifa wa Uruguay anatarajiwa kufanya makubwa ndani ya timu hiyo kuanzia msimu ujao.

