Mbivu na mbichi za Harry Kane na Spurs bado hazijajulikana, Nuno Espirito Santo kufanya mazungumzo na nahodha huyo baada ya Euro 2020.
Kuelekea mwishoni mwa msimu wa EPL, 2020/21, Harry Kane aliweka wazi lengo lake la kutaka kuondoka Spurs ikiwa ni lengo mahsusi la kutaka kubeba makombe. Suala hili lilizua taharuki miongoni mwa mashabiki na wadau wa soka.
Baada ya muda kupita, Daniel Levy aliweka wazi msimamo wake kuhusu Kane akisema wazi mchezaji huyo hatouzwa kwa gharama yeyote. Msimamo wa Levy unazingatia muda wa miaka 3 uliosalia kwenye mkataba wa Kane na Spurs.
Man City wamejipanga kutoa dau la £100M ili kumpeleka Kane Etihad Stadium, hata hivyo iliripotiwa Spurs wamekataa dau hilo na hawana mpango wa kusikiliza dau lolote kwa Kane.

Ujio wa Nuno unasuluhisha tatizo moja lililokuwepo kwa muda wa miezi 2 tangu kuondolewa kwa Mourinho. Japokuwa, matarajio ya mashabiki wa Spurs ni kuona timu hiyo inarejea kwenye utamaduni wake ikiwa ni sambamba na kufuatilia kwa ukaribu hatma ya Kane klabuni hapo.
Kane kwa sasa yupo na Timu ya Taifa ya Uingereza kunako mashindano ya Euro 2020 na amesema wazi kuwa hafatilii sana kinachoendelea Spurs na ameweka nguvu kubwa kwenye timu ya taifa kwa sasa. Baada ya mashindano ya Euro, wachezaji wote watakuwa huru kupumzika kabla ya kujiandaa na msimu ujao wa 2021/22.
Kwa namna ratiba zilivyo, inaripotiwa kuwa Nuno atafanya mazungumzo na Kane baada ya Euro na kabla ya mchezaji huyo kwenda likizo. Lengo kuu ni kutaka kujua muelekeo wa klabu ikiwa ni sambamba na kumsikiliza Kane kwa kile anachokihitaji kwenye safari yake ya kucheza soka. Je, ataendelea kubaki Spurs na kufanya kazi chini ya Nuno au anashikilia msimamo wake wa kutaka kuondoka?
IcyGems kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet. Ndio, ukiwa kwenye nyumba ya mabingwa, ndipo utakapoufurahia ubora wa Kasino ya Mtandaoni sambamba na kushinda kwa ushindi mkubwa! Ishi na hii, IcyGems!

