Ole Gunnar Solskjaer: Man United Tulipoteana

Kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amekubali kwamba timu yake ilipoteana na kucheza chini ya kiwango, tofauti na ilivyotarajiwa kwenye pambano la Jumanne la Ligi ya Mabingwa dhidi ya Young Boys.

Mashetani Wekundu wana kibarua cha ziada kwenye Kundi H, baada ya kukubali kichapo cha 2-1 dhidi ya Young Boys katika mchezo wao wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa, licha ya kuongoza mapema kupitia Cristiano Ronaldo.

Ole Gunnar Solskjaer: Man United Tulipoteana
Ole Gunnar Solskaer

“Tunajua matarajio ni makubwa na sisi wenyewe tunatarajia pia, uchezaji haukuwa wa kiwango chetu” Ole Gunnar Solskjaer alinukuliwa katika mkutano na waandishi wa habari Alhamisi.

Man United kwa sasa wanaongoza msimamo wa Ligi Kuu, na wataanza tena kampeni ya ligi ugenini dhidi ya West Ham United Jumapili.

Mashetani Wekundu pia wanatarajia kuchuana na West Ham kwenye Kombe la EFL Jumatano kabla ya kumaliza mwezi huku wakiwa na mechi za nyumbani dhidi ya Aston Villa na Villarreal kwenye ligi na Ligi ya Mabingwa.


MKWANJA NJE NJE NA DISCO FUNK

Unaanzaje siku yako na kuimaliza bila kupitia katika kasino bomba za meridianbettz, mchezo mashuhuri wa Disco Funk unaweza kukufanya uwe mshindi leo hii.!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe