Kiungo wa kimataifa wa kutoka nchini Ufaransa anayekipiga kwenye klabu ya Olympique Lyonnais Maxence Caquerest ameongeza kandarasi ya kusalia kwenye klabu hiyo mpaka mwaka 2027.

Maxence Caquerest kwenye maisha yake ya soka alinzaia kwenye akademi ya FC de Corbas ambapo alitumia mwaka mmoja tu kwenye akdemi hiyo na kuhamia kwenye kwenye akademi ya FC Chaponnay Marennes ambapo alitumia miaka mitano.

Olympique Lyonnais

Maxence Caquerest alisajiriwa na akedemi ya Olympique Lyonnais akitokea kwenye akedemi ya FC Chaponnay Marennes, baada ya kuitumikia miaka akademi ya Lyon kwa miaka tisa hatimaye mwaka 2019 alipandishwa kwebda timu ya wakubwa na kuanza safari yake ya soka la kulipwa.

Maxence Caquerest pia ameitumikia timu ya taifa Ufaransa kwa ngazi mbali mbali ambapo ameshaichezea timu ya taifa chini ya miaka 16,17,18,19,20 na 21. Lakini bado ameshindwa kufanikiwa kuichezea kwa ngazi ya timu ya wakubwa mpaka sasa.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa