Nyota wa klabu ya Juventus Paul Pogba amejibu vitisho vya ndugu yake Mathias kuwa anataka kuweka wazi kuhusu mambo ambayo watu wasiyoyajua kuhusu mchezaji huyo ili waamue, lakini Pogba alisema kuwa mamlaka za nchini Italia na Ufaransa zimeshapatiwa taarifa.

Mathias Pogba, ambaye amecheza soka la kulipwa nchi mbalimbali lakini kwa sasa hana timu baada ya mkataba wake kuisha na timu ya ligi ya daraja la nne nchini Ufaransa Belfort tangu mwezi April.

Paul Pogba, Paul Pogba Vitani na Ndugu Yake, Meridianbet

Mathias Pogba alichapisha video kwenye ukarasa wake wa Instagram akisema anataka kutoa ushuhuda mkubwa kuhusu kaka yake, wakala na mwanasheria Rafaela Pimenta pamoja na  Kylian Mbappe.

Paul Pogba kwenye waraka alioutoa siku ya Jumapili unasema: “Matamko ya hivi karibuni ya Mathias Pogba kwenye mitandao ya kijamii kwa bahati mbaya sio ya kushangaza.

“Wanakuja na vitisho na kujaribu kujipatia vitu na kundi liliojikusanya dhidi yangu. Hili tayari tumeshawasilisha mamlaka husika kwenye nchi zote mbili Italia na Ufaransa mwezi mmoja uliopita.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa