Pep Guardiola anasema anasema atawatumia vijana zaidi katika mechi dhidi ya Wycombe Wanderers kutokana na majeruhi yanayoendelea klabuni.
Aymeric Laporte, John Stones, Rodri na Oleksandr Zinchenko wote hao walikosekana jumamosi katika mechi ya ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Southampton, mechi iliyoisha pasipo timu yeyote kuona goli la mwenzie.

City italazimika kutowatumia baadhi ya nyota wao dhidi ya timu kutoka League One, huku wakijiandaa na safari ya kwenda Stamford Bridge tarehe 25 septemba.
Pep Guardiola alinukuliwa akisema “baadhi ya wachezji itabidi wapumzike kwa kusubiri mchezo ujao, Ruben Dias, Joao Cancelo wamecheza karibia mechi zote mpaka sasa, sidhani kama atawezacheza, na pia Gundogan sifikilii kama atacheza.”
“Hatuna mbadala tutahitaji kuwatumia vijana, ni nafasi nzuri kwa akademi kuweza kuonesha uwezo wao, kwanini maana wako pale,” aliongezea Pep Guardiola.
Baada ya kucheza na Wycombe, City watakutana na Chelsea, Paris Saint Germain kwenye ligi ya mabingwa na pia watacheza na Liverpool ndani ya siku tisa.
Ni wakati wa ushindi mkubwa ukiwa na kasino bomba ya Lock a Luck, meridianbet wanakupa sababu ya ushindi, funga bahati yako ya ushindi ukiwa na mabingwa.


