Kocha wa klabu ya Chelsea Mauricio Pochettino amemzungumzia mchezaji wake Nico Jackson kua ni kijana mdogo na hawatakiwa kumpa presha na watamsaidia kupata ubora wake.

Pochettino wakati anajibu swali la muandishi aliweka wazi kua ni kweli mshambuliaji huyo hayupo vizuri mpaka sasa, Lakini kuna mambo yamemfanya asifanye vizuri lakini hawapaswi kumtupa zaidi watamsaidia ili kukaa kwenye kiwango bora.pochettinoMshambuliaji huyo ambaye amejiunga na klabu ya Chelsea katika majira ya joto dirisha kubwa lililopita anaonekana kutokua kwenye ubora na mashabiki wa klabu hiyo wakiona hafai, Lakini kocha wake ameonekana kua na imani nae na kutaka apewe muda.

Kocha huyo wa zamani wa PSG amekua na kawaida ya kutetea wachezaji wake na kuamini wanahitaji muda zaidi haswa vijana, Kwani wiki kadhaa nyuma alieleza juu ya Mykhaylo Mudryk anahitaji kupewa muda zaidi ili kuonesha ubora wake.pochettinoKocha Pochettino imani yake juu ya wachezaji vijana imemlipa sana alipokua ndani ya Tottenham Hotspurs, Kwani aliwapa nafasi vijana kama Delle Ali, Harry Kane, na Kylie Walker na wakafanya vizuri sana hivo wengi wanaamini anaweza kufanya hivo pia kwa wachezaji hao wa Chelsea.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa