Kiungo wa Manchester United, Paul Pogba ametuma ujumbe ambao umeonekana kuwa ni kijembe kwa Legendi wa Manchester United, Gary Neville na Roy Keane ambao kwa pamoja walimtumia ujumbe kiungo huyo Jumamosi iliyopita kwamba anatakiwa kuachwa.

Nyota hao wa zamani wa Manchester United walisema kuwa ni muda sahihi wa United kumuacha Pogba aondoke ndani ya kikosi hicho kwa sababu wakala wake Mino Raiola alisema kuwa hana furaha ndani ya kikosi hicho.
Muda mfupi baada ya maoni hayo kwenye sare ya bila kufungana kwa Manchester United na Manchester City uliochezwa Uwanja wa Old Trafford, Pogba ambaye alianza pia kikosi cha kwanza alituma ujumbe kupitia ukurasa wake wa Istagram kwa kuwataka watu wasiojua mambo ya ndani kukaa kimya kwa kuwa hana tatizo na Manchester United.

“Muda wote napambana kwa ajili ya Manchester United, mashabiki na wachezaji wenzangu wote tunapeana sapoti. Bla bla sio kitu cha muhimu. Malengo yangu yapo mbali kila siku.
“Asilimia 1,000 ninahusika katika mipango kazi ya Manchester United, muda wote nimekuwa muwazi na kila kitu kinakwenda sawa. Ikiwa haujui kinachoendelea ndani usiongee,” .
MALIZA MWAKA KIBINGWA KWA KUJISHINDIA SHEA YAKO KWENYE SHILINGI 140,000,000TSH!!
Kipindi hiki cha sikukuu kinamalizika kwa namna ya kipekee. Shilingi 140,000,000 kushindaniwa katika michezo ya Evolution kwenye Kasino Mubashara ya Meridanbet. Ingia mchezoni na ujiwekee nafasi ya kushinda shea yako!!!



Khadija
sasa itakuwaje
Hopemwaikuka
Tumeumbuka huku
Shakila mrope
Mhh atari
Lydia Emmanuel Magoti
Duu sio poa
Sarah
Mh balaa
Sadick
Pogba mwenyewe na maneno ya wakala wake hayarandani, ni muda sasa kwake kuondoka Man U kutafuta malisho mengine mahali pengine
Ernest
Pogba bora asepe tuu ndani ya Man U
Ally mohamedi ally
Timu aieleweki bora aende
Caroline
Pogba anazingua
Dorophina
Pogba ni bora kuondoka tu man u haende akatafute kambi sehemu nyingine
Mwanahamisi
Pogba ni bora asepe
Issa
Pogba anajua kaz yake
Tatu
Pogba anajua anachokifanya
warda
Aondoke tu bwana mana anatuchezea vitu havieleweki
Rahma
Asepe tu
aisha
Duuh sio powa kabisa