Klabu ya PSG ya nchini Ufaransa imekua klabu ya hivi karibuni kufungua mazungumzo baada ya Real Madid ya kumsajili beki kisiki wa Chelsea, Antonio Rudiger, 28 ambaye mkataba wake na klabu hiyo ya London ukikamilika mwishoni mwa msimu.

Kulingana na jarida la BILD Rudiger amekataa mkataba mpya uliowekwa mezani na Chelsea, baada ya kumpa mshahara wa Euro 140,000 kwa wiki wakati mchezaji huyo akitaka Euro 200,000 kwa wiki.
Taarifa zinasema Wakala wa mchezaji huyo amesha fungua mazungumzo na mkurugenzi wa michezo wa PSG, Leonardo kwaajili ya usajili wa beki huyo.
Rudiger ambaye anaingia katika miezi 6 ya mwisho ya mkataba wake pia amehusishwa na klabu ya Real Madrid, Barcelona na Manchester United ambao wameonyesha nia endapo atashindwa kuongeza mkataba.
Antonio Rudiger amedumu Chelsea kwa miaka mitano akiwa ameisaidia timu hiyo kutwaa kombe la FA, Europa League na UEFA Champions League katika kipindi hicho.
Fanya wiki yako iwe ya ushindi mkubwa ndani ya kasino za mtandaoni za meridianbet. Mchezo wa BURST THE BANK🔥🤑 ni moja kati ya mchezo pendwa unaowapa wachezaji mamilioni kila siku. Kwa dau dogo unashinda zaidi.


