Mlinzi wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa Hispania ambaye ana rekodi zake nyingi sana katika soka, Sergio Ramos aliweza kufika katika hatua kubwa sana kisoka mara baada ya mechi yake dhidi ya Faroe Island. Hatua hiyo iliweza kufikiwa mara baada ya kupitia katika kipindi cha misukosuko katika safari yake ya kisoka.
Lengo la nyota huyo ni kufikisha michezo 200 kama alivyokaririwa akisema kwa kinywa chake, anaonelea kwamba hiyo ni hatua ambayo anatamani sana kuweza kuifikia kisoka mara baada ya kuvunja rekodi kadha wa kadha ndani na nje ya uwanja akiwa kama mchezaji wa nafadi nyeti sana.
Hadi sasa ameweza kulingana na Cassilas wakiwa ni wachezaji ambao wameweza kufikisha jumla ya mechi 167 ndani ya taifa hilo huku kukiwa bado na mwendelezo wa yeye kuonekana uwanjani akifanya maajabu yake. Na kwa uwezo wake na umri wake bado ana safari nyingine ya kuendelea kuonekana na kikosi hicho.
Baada ya kulingana na Cassilas mchezaji huyo aliweza kuzungumzia hatua hiyo kwa kusema kwamba mara zote rekodi zimewekwa ili zivunjwe na anajiona mwenye furaha kubwa sana kuweza kufanikiwa kuivunja rekodi hiyo jambo ambalo akiwa kama mchezaji anakuwa analitamani sana. Maisha yake ya soka la kutambulika na dunia aliyaanza 2005.
Anaonelea kwamba kwa kasi aliyonayo, matamanio na matarajio anayoyaangazia ni wakati mzuri sana kwake kuweza kujenga rekodi kubwa kwa alama isiyofutika. Anaona kwamba akifanikiwa kufikia hatua hiyo ya michezo 200 itakuwa ni hatua ya pekee sana kwake katika mafanikio ya soka.
Cassilas ambaye alikuwa tayari kwenye nafasi ya idadi hiyo ya michezo ameweza kumtumia salamu za pongezi nyota huyo kwa hatua hiyo kubwa ambayo ameweza kuifikia hadi sasa. Pia amemkaribisha katika kitabu chake cha historia ambacho wanakijenga ndani ya taifa hilo la Hispania.
Ramos ambaye ni mshindi mara mbili wa kombe la Ulaya 2008 na 2012 na kombe la dunia 2010 aliweza kushukuru kutokana na ujumbe ambao Iker aliuweka kumsifu kwa hatua hiyo kubwa. Hadi sasa amefanikiwa kuiweka katika nafasi nzuri timu yake ya taifa katika michuano ya kufuzu kucheza Euro 2020.


Rehema Dickson
kwa kasi aliyonayo, matamanio na matarajio anayoyaangazia ni wakati mzuri sana kwake kuweza kujenga rekodi kubwa kwa alama isiyofutika. Anaona kwamba akifanikiwa kufikia hatua hiyo ya michezo 200 itakuwa ni hatua ya pekee sana kwake katika mafanikio ya soka.
Fatina mfingi
Makala nzur