Mkongwe wa klabu ya Real Madrid ambaye aliacha historia kubwa kikosini hapo, Luis Figo anaonelea kwamba nyota wa muda mrefu na kiongozi wa wachezaji uwanjani na kikosini hapo Sergio Ramos anastahili kabisa kuheshimiwa na kupewa tuzo ya Ballon d’Or kutokana na mchango wake aliouonesha kikosini hapo na kwenye timu yake ya taifa.
Ramos [32] ni mchezaji aliyejenga historia kubwa kikosini hapo kwa wakati uliopo na kwa kipindi cha nyuma tangu ajiunge na klabu hiyo. Hadi sasa ameisaidia klabu hiyo kuweza kunyanyua takribani makombe manne ya klabu bingwa ya dunia; akiwa na wazee wa Los Blancos kitu ambacho kinamfanya azidi kuonekana bora zaidi.
Baadhi ya vitu vinavyoshawishi Ramos aonekane bora zaidi ni kama vile; tangu anunuliwe na klabu ya Real Madrid akiwa kama mchezaji wa Sevilla kipindi hicho miaka ya 2005, Ramos amekuwa mhimili mkubwa ndani ya kikosi hicho jambo ambalo limeonwa na kila shabiki wa soka kwamba nafasi yake ni kubwa mno.
Raia huyo wa Hispania hadi sasa anahusika katika michezo 604 aliyoicheza ndani ya klabu hiyo hadi sasa huku akiwa amefanikiwa kufumania nyavu mara 84 katika nafasi yake ya ulinzi na akiweza kutoa pasi za magoli 39; jambo ambalo ni mageuzi makubwa kwenye soka kwa mtu wa nafasi yake anayocheza kuweza kufanya hivyo.
Hadi wakati huu ameweza kushinda makombe makubwa kumi [10] hayo yote yakiwa ni kwa ngazi ya klabu, kombe la dunia pia kombe la Ulaya akiwa na timu yake ya taifa ya Hispania. Hayo ni baadhi tu ya makubwa aliyoyafanya akiwa na klabu yake hiyo na athari zake kushuhudiwa moja kwa moja hata katika ngazi ya taifa.
Msimu uliopita aliiongoza klabu yake hiyo ha Madrid katika kugombania taji la tatu mfululizo la klabu bingwa Ulaya na ni jambo ambalo alifanikisha akiwa na kikosi hichohicho cha Madrid. Japo baadaye hawakufanya vizuri kwenye kombe la Dunia. Jambo ambalo lilionekana kuwa gumu kwa kikosi hicho kutokana na kukosa ushindani.
Figo yeye anaona kwamba Ramos anastahili na ana kila haki kuipata hiyo kutokana na msaada mkubwa aliounesha tangu alipoanza maisha yake ya soka la kulipwa hususani kwenye klabu kama hiyo yenye ushindani mkubwa na yenye uwezo kwa kufanya biashara wakati wowote kama wanakuwa wamepata kile wakichokihitaji. Hayo ni mambo yanayompa nafasi hiyo kutokana na mchango kwake huo.
Kuwa mlinzi ni changamoto sana kushinda tuzo hiyo kama ilivyo kwa golikipa jambo ambalo kwenye historia ya karinuni tangia kichukuliwe na Cannavaro. Japo hili hutegemeanna na mwaka husika na ushindani ulipolalia kwa kipindi hicho. Ramos amepitia kila aina ya kipindi akiwa Madrid ikiwemo vipindi vya matunda hata vile vya mpito ndio mana Figo anaona kwamba nyota huyo anastahili zaidi ya hapo.
Zeiyana
Kweli anacho sema figo Ramos ni mchezaji ambaye hana stori kubwa sana real Madrid