Baada ya Kocha wa Hispania, Luis Enrique kuwasilisha orodha ya wachezaji 24 walioitwa kwenye Mashindano ya Euro, ambapo stori kubwa ni kuacha kumjumuisha nahodha wa Real Madrid, Sergio Ramos.

Ramos amesema: “Baada ya msimu mrefu wa mapambano na ugumu nakiri kuwa nimepitia mengi magumu na hili la Euro linaingia.
“Nimepambana kama ilivyo siku zote kwa mwili na nafsi yangu ili nirejee kwenye ubora wangu kwa 100% kwa ajili ya klabu na timu yangu ya Taifa ila sio kila muda mambo huwa vile tunadhani.
“Imeniuma sikuweza kuisaidia Real Madrid na kuipambania timu yangu ya Taifa, lakini sina budi kupumzika ili kurejea vyema kwa ajili ya klabu na Taifa langu.
“Kutoka moyoni nawatakia kheri Wachezaji wenzangu wa timu ya Taifa, nami nitakuwa nyumbani kuishangilia timu kama Watu wengine, kila la kheri Hispania.”
BONASI YA 50% KILA SIKU KATIKA KASINO ZA EVOPLAY HAPA MERIDIANBET.
Meridianbet na Evoplay Kasino wanakupa bonasi ya 50% ya kiasi utakachoweka katika akaunti yako leo. Unasubiri nini ni wakati wa kupiga pesa sasa na Mabingwa.
Majanga
Hatari