Hatimaye rekodi na historia kubwa imeandikwa baada ya Azam Media Group kusaini mkataba na shirikisho la soka TFF wa kuendelea kuonesha mechi za ligi kuu kwa miaka 10, huku thamani ya mkataba huo ikiwa ni bilioni 225.6.
Azam Media imekuwa ikirusha matangazo ya Ligi kuu tangu mwaka 2013, na hivi karibuni imekuwa ikijihusisha na matangazo hayo kwa muonekano mzuri huku kila mwaka ikiboresha teknolojia yake ili kuwafikia watu wengi zaidi.
Udhamini huu wa kuonesha matangazo ya mechi za mpira wa miguu katika VPL umeambatana na faida nyingine nyingi sana kwa timu shiriki na zile zitakazoshinda ubingwa wa VPL.
Kwa misimu mitatu ijayo tu,
Bingwa wa VPL – 500M
Mshindi wa Pili – 250M
Mshindi wa Tatu – 225M
Mshindi wa Nne – 208M
Licha ya hayo tu kwa msimu ujao tu Azam Media imetangaza kutoa takribani bilioni 8 kwa timu 16 shiriki za ligi kuu bara, yaani kwa wastani ni kama milioni 500 kwa kila timu. Jambo hili limeungwa mkono na wadau wengi wa soka na ni kitu ambacho kinaipa thamani ligi ya Tanzania.
BONASI YA 50% KILA SIKU KATIKA KASINO ZA EVOPLAY HAPA MERIDIANBET.
Meridianbet na Evoplay Kasino wanakupa bonasi ya 50% ya kiasi utakachoweka katika akaunti yako leo. Unasubiri nini ni wakati wa kupiga pesa sasa na Mabingwa.
Kila la kheri Azam