Miongoni mwa maamuzi mazito yanayosubiriwa Manchester United, ni kocha atakayekabidhiwa timu. Ralf Rangnick ananguvu yake katika hili. Fergie Je?
Manchester United waliachana na Ole Gunnar Solskjaer baada ya matokeo mabovu msimu huu. Kuondoka kwa Ole kukafungua milango kwa Ralf Rangnick kupewa timu kama kocha wa muda (mpaka mwishoni mwa msimu).
Baada ya miezi 6 ya kuiongoza United, Ralf atapanda ngazi na kuhusika zaidi kwenye nafasi za ushauri wa kimichezo ndani ya klabu hiyo. Kazi ya kwanza ikiwa ni kumpata kocha wa muda mrefu.
Sir Alex Ferguson amekuwa na nafasi kubwa kwenye uteuzi wa makocha toka alipostaafu nafasi hiyo mwaka 2013. Fergie ndiye aliyemchagua David Moyes kama mrithi wake. Baadae wakaja Lois Van Gaal, Jose Mourinho na Ole Gunnar Solskjaer. Wote, hawakutimiza lengo la Man United (kutwaa ubingwa wa EPL).
Inasemekana, Fergie anampigia upatu Mauricio Pochettino kuwa kocha wa United. Alianza kufanya hivi toka 2016 wakati Mourinho akiwa kwenye nafasi hiyo. Swali ni je, mkeka wake utatiki safari hii?
Ralf Rangnick bado hajashawishika kama Pochettino ndio mtu sahihi kuiongoza United baada yake. Inasemekana, Ralf anampa nafasi zaidi Erik Ten Hag kuliko Pochettino. Uongozi mpya chini ya Richard Arnold na kuongezwa kwa Ralf kwenye kitengo cha maamuzi, huenda kukachana mkeka wa Fergie ambaye amekuwa akisikilizwa sana na wafanya maamuzi wa United.
Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.
CHEZA HAPA