Ronaldo: Nilikuja Man United Kushinda Mataji

Nyota wa klabu ya Manchester United Christiano Ronaldo anaamini timu hiyo inaweza kufanya vizuri na kumaliza katika nafasi za juu katika ligi kuu ya Uingereza na amesisitiza Ralf Rangnick apewe muda ili kuiweka timu kwenye muelekeo mzuri.

Ronaldo: Nilikuja Man United Kushinda Mataji

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36 alirejea klabuni mwaka uliopita kwa shangwe na matarajio mengi, lakini msimu umekua mbaya kwa Mashetani Wekundu, huku timu ikishindwa kufanya vyema chini ya Ole Gunnar Solskjaer – ambaye alitimuliwa Novemba.

“Sikuja hapa ili kuwa kwenye nafasi ya sita, au nafasi ya saba, au nafasi ya tano,” Ronaldo aliambia Sky Sports.

“Niko hapa kujaribu kushinda mataji, kushindana.

“Nadhani ili kujenga vitu vizuri, wakati mwingine lazima uharibu vitu vichache.

“Kwa hivyo kwa nini isiwe – mwaka mpya, maisha mapya na ninatumai kuwa Manchester United inaweza kuwa kiwango ambacho mashabiki wanataka. Wanastahili hilo.

“Tuna uwezo wa kubadilisha mambo kwa sasa, najua njia lakini sitaitaja hapa kwa sababu sidhani kama ni uadilifu kwa upande wangu kusema hivyo.

“Ninachoweza kusema tunaweza kufanya vizuri zaidi – sisi sote. Manchester United ni ya vitu muhimu, kwa hivyo tunapaswa kubadili hilo.

“Nadhani tunashindana lakini bado hatujafika katika kiwango chetu bora. Lakini tuna safari ndefu ya kuimarika na ninaamini tukibadilisha mawazo yetu, tunaweza kufikia mambo makubwa.”


JIACHIE NA ALMIGHTY AZTEC

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe