Kocha wa klabu ya Brighton Hove Roberto De Zerbi anaamini timu ya Tottenham Hotspurs ina uwezo kua mabingwa wa ligi kuu ya Uingereza msimu huu.
Roberto de Zerbi ambaye anakwenda kucheza dhidi ya Tottenham ya Antonio Conte kesho jumamosi katika dimba la nyumbani la Amex kwa mara ya kwanza toka kocha huyo achukue mikoba ya Graham Potter alietimkia jijini London katika klabu ya Chelsea.
Klabu ya Brighton endapo itashinda mchezo wa kesho inaweza kukwea hadi nafasi ya tatu kwakua iko nyuma ya Purs wanayocheza nayo kesho kwa alama tatu hivo idadi ya maholi inaweza kuwaeka nafasi ya tatu Brighton au wakabaki nafasi ya nne huku wakiwa na kiporo mkononi.
Akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari leo ijumaa Roberto de Zerbi amesema “Nafikiri vijana wa Conte bado wanaweza kupambana,Nadhani Tottenham wako kwenye hali nzuri ya kushinda ligi”
“Sio rahisi kwasababu kuna City,Liverpool,Chelsea, Lakini kwenye dirisha la usajili lililopita walinunua wachezaji wazuri sana, N a baada ya kufanya kazi mwaka mmoja na Conte wanaweza kushinda ligi” Alisema De Zerbi
Kocha huyo aliendelea kuisifu Spurs kua ni timu bora kwakua haina kikosi cha wachezaji 11 tu kwani wanaweza kua wachezaji bora lama 20 au 22 na kusisitiza timu hiyo imekua bora zaidi ya mwaka mmoja au miwili iliyopita.

