Sakata la staa wa klabu ya Paris Saint German ya nchini Ufaransa Klian Mbappe linachukua sura mpya kadri siku zinavyokwenda. Nyota wa zamani wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Uingereza Wayne Rooney ametoa maoni yake juu ya hali ya mchezaji huyo ndani ya klabu yake,Pia kueleza tukio lililotokea mwisho wa juma lililopita kwenye mchezo ulioihusisha klabu ya PSG dhidi ya Montpellier ambapo klabu ya PSG walipata ushindi wa goli tano kwa mbili.

Kupitia mechi hii ndiyo iliyoibua mzozo mpaka leo hii ambapo Mbappe alikosa mkwaju wa penati wa kwanza uliopatikana kwenye mchezo huo.Ila hali ilibadilika ilipotokea penati ya pili ambapo Mbappe alihitaji kupiga tena lakini wakati huu staa mwenzake wa klabu hiyo Neymar Jr alimgomea na kupiga mkwaju ule na kufunga.Mbappe, Rooney Amuwakia Mbappe., MeridianbetBaada ya tukio hilo Mbappe alionekana kukerwa na kumgonga staa mwingine wa timu hiyo Lionel Messi begani wakati anaondoka eneo hilo,Hali iliomfanya Wayne Rooney kuzungumzia tukio na kuoneshwa kukerwa na kusema hivi “kijana wa miaka 22/23 anamgonga Messi begani sijawahi kuona kiburi kama hichi kwenye maisha yangu” Na kutaka Mbappe akumbushwe wakati Messi ana umri kama wake alikua tayari ana ameshinda Ballon d’or mara nne.

Kutokana na maelezo hayo ya gwiji wa zamani wa vilabu vya Man United na Everton inaonesha fika anamtaka Mbappe kuacha kiburi na kumuheshimu Messi kwani kijana huyo hajafanya hata nusu ya aliyoyofanya Messi kwenye dunia ya mpira.

Siku kadhaa sasa ndani ya klabu ya PSG kumekua na kutokuelewana baina ya Mbappe na wachezaji wenzake,Ni baada ya kugundulika mkataba aliosaini Mbappe wa kumbakiza klabuni hapo mwishoni mwa mwezi Mei mwaka huu ulikua unamfanya mchezaji huyo kua na mamlaka makubwa ndani na nje ya uwanja. Jambo lililowakera wachezaji wenzake ndani ya klabu na kuleta mpasuko mkubwa ndani ya timu hiyo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa