Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Uingereza Wayne Rooney ametangazwa kua kocha mpya wa klabu ya Birmingham City.
Rooney ameteuliwa kuiongoza Birmingham City baada ya siku chache kuachana na klabu ya DC United inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Marekani na sasa amesaini mkataba wa miaka mitatu wa kuitumikia Birmingham.Wakati wa utambulisho wake kama kocha mpya wa Birmingham City mfungaji bora huyo wa muda wote wa Man United alisema “Nimefurahi kua hapa. Ni wazi kabisa wana mpango,Ni mradi ambao unanipa hisia za dhati kabisa na nina hamu ya kuanza kufanya kazi hapa”
Mchezaji huyo ambaye amechukua nafasi ya aliyekua kocha wa klabu hiyo John Eustace ataungana na wachezaji wenzake wa zamani katika benchi la ufundi la klabu hiyo ambao watakua beki John O’shea ambaye alikipiga nae ndani ya Man United na Ashley Cole ambaye walicheza pamoja timu ya taifa ya Uingereza.Wayne Rooney anaenda kufundisha klabu yake ya tatu baada ya kuanza majukumu ya ukocha rasmi, Kwani mshambuliaji huyo alishafanikiwa kufundisha klabu ya Derby County,na Birmingham City inayoshiriki daraja la pili nchini Uingereza.