Safari ya Mo Ibrahim na Wimbo wa Mfalme

Ni mara chache sana Msanii kutoka Tanga akaja Mzizima kisha akaimba visivyoeleweka, niliwahi kumsikia Khamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ na mitaa ikamuita Choir Master, kabla hata ya Roma Mkatoliki, am happy to say wanajua wanachoandika

Nilianza kuliona anguko la MO Ibrahim pale Msimbazi kabla hata ya majuto ya Shiza Kichuya, nilikuwa na sababu zaidi ya billion kusema hivyo, am sorry to say this kwakuwa sikuweza kumfikia na kumwambia wapi anakosea, am sorry once again

Maarifa ambayo Mwana FA aliyosema amepewa na Mfalme, ndio maarifa ambayo MO alipewa na Mfalme huyo huyo, ndipo maarifa ya kusakata kabumbu kwenye eneo la kiungo pale Mtibwa Manungu Turiani, miguu yake ikamtoa pale Mzizima na kusaini Simba, maarifa yalimpa nyadhfa

Kwenye chorus ya Mfalme, G NAKO alisema maarifa yalimpa nyadhfa kisha akaziba nyufa, Naam MO Ibrahim aliikuta Simba inachechemea sana, hakuna michuano ya Kimataifa ndani ya miaka kadhaa, lakini kipaji chake kiliwapeleka FA pale Dodoma

Kuna kitu alikisema tena FA kuhusu kuutunza mziki mzuri ‘Keeping the good music alive’, hata MO alikuwa anakifanya pale dimba la Uhuru, atapokea mpira atakavyo, atageuka atakavyo, atapiga pass atakavyo na kufunga atakavyo, ndani ya Simba alikuwa Lulu kubwa mno

Nadhani tulishawasha taa ya kijani kwa MO Ibrahim kuwa anaenda kufikia hatua kubwa kama Mbwana Samata ambae aliwahi kupita hapo, ila mwishoni mwa msimu wa 2016/17 haikuwa vile tulivyofikiria, kiukweli Mungu ana maguvu sana

Leo hii naamka nakumbuka MO alikuwepo kwa mkopo Namungo FC na hakucheza kabisa, naamka asubuhi kugundua kipaji kile sio ambacho kilimfanya Thobias Kifaru avimbe au Simba watambe, kiukweli nikakumbuka Mwana FA alisema unapata ulichoandikiwa, Mungu hakupi kama hataki

Lakini katikati ya machozi yangu naamini hata MO analia sasa hivi, ila hapaswi kulalamika hana viatu kwakuwa kuna wenzie hawana miguu, hapaswi kulia kwakua yupo Kagera kujaribu tena huku wengine hata timu hawana hivi sasa, asilie

Mwana FA alisema Yule Mfalme wetu ndie ana mipango, angetaka angetuumba Fungo na hatupaswi sana kuhukumu ni kazi yake Mfalme.


Beti kwa Kitochi Kushinda 300,000,000!

Unajua kuwa unaweza kushinda milioni mia tatu kwa buku tu? Ndiyo! Unaweza kushinda kwa kupiga *149*10# na kubashiri. Ingia mchezoni!

Soma Zaidi

35 Komentara

    Ibrahim yupo vizuri sana akiwa uwanjani

    Jibu

    mo ibrahim ni kijana mdogo mwenye uwezo mkubwa awapo uwanjani

    Jibu

    Ni mchezaji mzuri sanameridianbett#

    Jibu

    Maisha ndivyo yalivyo leo vile kesho vile. Dogo Tariq aliiuzwa na Chelsea kwenda Brighton kwa fedha kiduchu na leo Bayern inamutaka kwa mamilioni ya Dollar. MO akaze tu huko aliko#meridianbettz

    Jibu

    Mwandiko bora kabisa ndugu mwandishi

    Jibu

    Hii Ni makala nzuri mashabiki tunafurahia

    Jibu

    Nlkua cjui hii

    Jibu

    Asante kwa taarifa

    Jibu

    Mo ibrahim amepotea mapema kwenye football

    Jibu

    Mchezaji bora kabisa.

    Jibu

    Asanteh meridianbet kwa kitujuza

    Jibu

    Huyo mchezaji ni hatar sana

    Jibu

    Hii inaitwa kipaji bila jitihada nothing

    Jibu

    Kijana yupo vizuri

    Jibu

    Mchezaji noma sana

    Jibu

    Uyo mchezaji anajituma sana

    Jibu

    Goodupdate

    Jibu

    Mwana FA ana mistari adi raha

    Jibu

    Kijana yupo vizuri

    Jibu

    Mo yupo vizuri

    Jibu

    Ibrahim yupo vzr sana

    Jibu

    Mo ibrahim amekuw kama amepotea kwenye game

    Jibu

    Mchezaji mzuri

    Jibu

    Mchezaji mwenye kipaji lakn ajitumi km anaetak mafanikio

    Jibu

    Ibrahim yuko vzr sana

    Jibu

    Mo Ibrahim ni mchezaji makini sana

    Jibu

    Ibrahim nimchezaji mzuri

    Jibu

    Mo Ibrahim amekua kama kapotea kwny game

    Jibu

    yupo vizuri

    Jibu

    Mo lbrahim nikijana mdogo mwenye uwezo akiwa uwanjani anajua mpira

    Jibu

    Kupotea kwa mchezaji kutokana na jinsi mwenyewe anavyojituma juhudi zinaitajika

    Jibu

    Basi tujikumbushe na ule mstari unaosema “Kuna vingi vya kumuomba Mungu kabla hujamuomba utajiri”

    Jibu

    Mwamba yupo vizuri

    Jibu

    Basi tujikumbushe na ule mstari unaosema “Kuna vingi vya kumuomba Mungu kabla hujamuomba utajiri”

    Jibu

    Habar njema

    Jibu

Acha ujumbe