Samatta na Wenziye Kuanza Kampeni…

Baada ya majadiliano ya muda mrefu juu ya ni lini ligi ya EPL irejee, ligi ambayo mwanzo ilipangwa kurejea Juni 12, sasa ni rasmi kuwa ligi hiyo itarejea mnamo Juni 17 baada ya vilabu vyote kukubaliana hivyo.

Ligi hiyo itaanza kwa Aston Villa ya Samatta kuwakaribisha wageni Sheffield United, huku Manchester City wakiwaalika Arsenal pale Etihad Stadium. Mechi hizi mbili ni muendelezo wa kukamilisha viporo ili timu zote katika ligi kuu ziwe zimekwishacheza michezo 29 kisha ligi hiyo itaendelea tena June 19 na 21 katika raundi yake ya 30.

Timu ya Aston Villa anayochezea nyota wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta itarudi uwanjani kuendeleza harakati zake za kujinusuru kutoka katika wimbi la kushuka daraja wakiwa na kumbukumbu mbaya ya kuraluliwa vibaya na Leicester City katika kipigo cha aibu cha 4 kwa sifuri katika mchezo wao wa mwisho, na ikumbukwe kuwa huo ndiyo ulikua mchezo wa mwisho wa ligi ya Primia kabla haijasimamishwa kwa ajili ya janga la Corona.

Aston Villa walio katika nafasi ya 19 ya msimamo wa ligi yenye jumla timu 20 watakua na kibarua kizito mbele ya Sheffield United ambao wao wapo katika nafasi ya 7 huku wakiwa wamejikusanyia jumla ya alama 43. Hakuna namna nyingine kwa Samatta na wenzie kujinusuru wasishuke daraja ila tu kwa kushinda mchezo huo na mingine itakayowakabili.

Aston Villa wenye jumla ya alama 25 katika michezo 19 waliyocheza mpaka sasa, wamebakiwa na michezo 10 mkononi ambayo wanatakiwa kufanya wawezavyo wabaki katika ligi kuu. Kitu pekee kinachoonekana kuwa kinaweza kuwarahisishia Aston Villa kubaki katika ligi hiyo ni kujikusanyia alama zaidi ya 15 ili wawe na jumla ya alama 40 kujihakikishia nafasi yao katika EPL.

Ni Kwanini Alama 40 Zinaweza Kuwa Salama Kwao?

Katika misimu 23 ya ligi kuu ya Uingereza maarufu kama ‘EPL’ kuna jumla ya timu 20 zilizowahi kushushwa daraja, katika hizo ni timu tatu tu ambazo zilishuka zikiwa na alama kuanzia 40.

Kwa zaidi ya miaka 15 sasa hakuna timu iliyoshuka daraja kutoka Primia ikiwa na alama kuanzia 40. Kumbukumbu zinasema kuwa timu ya mwisho kufanya hivyo ni West Ham United ambao walishuka daraja msimu wa 2002/03 wakiwa na alama 42.

Kwa mazingira hayo, ni wazi kuwa alama 40 ndiyo salama kwa Samatta na wenzie ili waweze kusalia ndani ya ligi kuu, Vinginevyo safari yao ni ya mashaka.

43 Komentara

    sisi mashabiki wa EPL nasubiri kwa hamu yi tarehe 16

    Jibu

    Litakuwa jambo la kusikitisha endapo Aston Villa itashuka daraja. Hamu yangu ni kuona Liverpool anachukua Ubingwa#meridianbettz

    Jibu

    Eeeh! Ni hatari sisi mashabiki tunasubili hiyo siku

    Jibu

    Macho modo kwa ajil ya hyo siku

    Jibu

    Tunaisubiri hiyo siku

    Jibu

    Nasubiri kumuona samagoal77

    Jibu

    Wapenzi wa soka tunasubir kwa hamu

    Jibu

    Wapenzi wake wanatamani kumwona EPL lakini kuna hati hati ya timu yake kushuka daraja

    Jibu

    Ahsanteni kwa makala safi

    Jibu

    EPL kuna hati ya Kushuka daraja

    Jibu

    wanatamani kumwona EPL lakini kuna hati hati ya timu yake

    Jibu

    Anakibarua kizito sana samatta mana timu iko mkiani kabisa na watanzania tuna kiu ya kuendelea kumuona Epl

    Jibu

    Sisi Kama mashabiki
    Tunaisubiri kwa hamu

    Jibu

    Wapige tizi tu maana ninapomuona mtoto wa mbagala huwa nafrahi Sana anpopiga free after zake hatari tupu

    Jibu

    Mungu ibariki Aston villa ili samatta na wenziye waendelee kusalia katika ligi.

    Jibu

    Tunaimbea Aston villa ijitahidi isishuke daraja..maana jembe letu mbwana samata tunamtegemea sana.

    Jibu

    Astonvilla itakuwaje sasa kama itatoka kwenye ligi duh

    Jibu

    Ni habari mbaya kwa kweli

    Jibu

    hamu yangu kubwa kumuona samagoal77

    Jibu

    Wajitahidi tu wasishuke daraja#Meridianbettz

    Jibu

    Da! Kweli ni habari njema

    Jibu

    Hii sio nzuri kwa upande Wa samatha

    Jibu

    Kwa Jack Grealish yule dah tutarajie wakishuka tu daraja

    Jibu

    Natak kumuona sama goal atafanya nn epl

    Jibu

    mambo n moto tumemis sana
    mitupio sammagoal

    Jibu

    Habari njema

    Jibu

    EPL ndo mwake tunaisubir kwa ham

    Jibu

    Mambo ni Moto#meridianbettz

    Jibu

    Wajitaidi wasishuke daraja

    Jibu

    Habari mjema

    Jibu

    Hakuna namna nyingine kwa Samatta na wenzie kujinusuru wasishuke daraja

    Jibu

    Kitaani panaanza kuchangamkaaa

    Jibu

    Ni vizuri sana kama samatta atakuwa fiti ili aendelea kuwapiga magoli makipa wa timu kubwa

    Jibu

    hahaha jamani arsenal mmsimpigie hesabu na city anafungwa nyingi tu arteta hawezi kumzuia boss wake sama goal king of header ana kamba yake ya header

    Jibu

    Samagoal! Pambania timu yko
    Bado tunakuhitaji EPL

    Jibu

    Iko poa hiyo

    Jibu

    Natak kuwaona Aston villa watabaki epl au watashuka daraja thnks meridian bet

    Jibu

    Tarehe 17 June ndani ya EPL kutanoga sana, Huku Samatta kule Aguero

    Jibu

    Samatta piga mpira tunakusubiri kwa hamu zote

    Jibu

    Aston villa inaitaji ipambane ili isishuke daraja.

    Jibu

    Daaaah inauma sana wakija shuka daraja mana mbagala ndio wapezi wakubwa wa timu ya mbwana samatta

    Jibu

    Hiyo tarehe yenyewe tunaona km inachelewa kufika mambo yanogeee

    Jibu

    Was was wangu tu ipo kweny Tim kushuka daraja

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.