Sanamu ya nguli wa NBA Kobe Bryant na mwanae Gianna Gigi Bryant imepelekwa kwenye eneo la ajali ya helikopta ambapo walipoteza maisha pamoja na wengine saba kwenye mlima karibu na Los Angeles miaka miwili iliyopita.
Sanamu hiyo ya shaba yenye uzito wa kilo 73 inaonyesha wawili hao wakiwa wamevalia vifaa vya mpira wa vikapu na kutazamana kwa upendo huku Gigi akiushika mkono wa Kobe akiwa ameuweka begani mwake.
Mchongaji sanamu Dan Medina alikuwepo kuwasalimia mashabiki waliosafiri umbali wa maili 1.3 kutoa heshima zao kwa nguli huyo wa michezo.
“Haya yote nimeamua mwenyewe, hakuna aliyeniomba nifanye,” alisema Madina.
“Siku hii, maadhimisho ya pili ya ajali, niliamua kuileta kutoka mawio hadi machweo ya jua na kutoa wa uponyaji kwa mashabiki.
“Leo ilikuwa ya siku ya kipekee kwa sababu nilishuhudia mengi. Watu wamekuja na wameondoka wakiwa wameridhika.”
Yaliyochorwa kwenye msingi wa chuma cha sanamu hiyo ni majina ya waathiriwa tisa wa ajali ya asubuhi katika hali ya hewa yenye ukungu mnamo Januari 26, 2020. Inajumuisha pia maandishi ya nukuu maarufu ya Bryant: “Mashujaa huja na kuondoka, lakini hadithi ni za milele.”
Bingwa mara tano wa NBA katika misimu yake 20 akiwa na Los Angeles Lakers, kifo cha Bryant akiwa na umri wa miaka 41 kilishtua ulimwengu wa michezo ya kulipwa na kupelekea mashabiki wake wengi kuomboleza.
Gigi alikuwa na umri wa miaka 13 wakati wa ajali hiyo, ambayo ilitokea walipokuwa wakielekea kwenye mashindano ya vijana ya mpira wa kikapu.
Dakika tano pekee zinakutosha kuwa mmoja wa washindi wa mkwanja mrefu ndani ya kasino pendwa ya meridianbettz katika sloti maridhawa ya KENO, moja ya michezo inayoipa thamani dau lako.