Kocha wa Chelsea ambaye anakiongoza kikosi cha mabingwa hao wa UEFA Europa League amekuwa na nafasi ya pekee sana kupata nafasi ya awali kutua ndani ya klabu ya Juventus ambapo amekuwa na nafasi hiyo kubwa sana baada ya kuwapiku wenzake akiwemo Guardiola na Conte.
Guardiola aliitema ofa ya kuifundisha klabu hiyo kwa kuona kwamba bado ana nafasi kubwa ya kuendelea kusalia ndani ya klabu ya Manchester City ambao kwa nafasi kubwa tayari amewaonesha radha ya mafanikio kwa nafasi kubwa sana ndani ya kipindi cha muda mfupi.
Sio jambo jipya kwa kocha wa aina hiyo kupiga chini ofa nono kama hiyo kutokana na vile ambavyo kikosi chake cha mwanzo amekijenga tayari. Kuanza upya sio jambo jepesi ndiyo maana makocha wengi hupenda kusalia ndani ya kikosi fulani kwa kipindi kirefu sana ili kuweza kuweka muunganiko mzuri ndani ya kikosi.
Juventus tayari wameshinda taji la ligi kwa mara ya nane mfulilizo ndani ya ligi hiyo. Jambo hili ni matunda ya pekee ya kocha wa mwanzo, Allegri ambaye kwa nafasi kubwa amekipa nafasi kikosi hicho ya kuweza kutamba na kuuza ndani ya soka huku akiwa na majina makubwa kama Ronaldo.
Zile ripoti za awali ambazo zilikuwa zikimhusisha kocha huyo kuachana na Chelsea zinaonekana kuwa na uhalisia wa aina fulani baada ya kuwepo kwa maamuzi sahihi ya kutaka kukijenga kikosi chao pamoja na kuwa hawajapewa uhuru wa kufanya usajili kutokana na makosa waliyoyafanya hapo awali.
Tetesi za mwanzo zilikuwa kwamba Pep angejiunga na klabu hiyo baada ya kuwapa taji City ambao bado hajapata nafasi ya kufanya vizuri kwenye michuano mikubwa kama ile ya ligi ya mabingwa. Inaonekana wamekubaliana kipindi cha miaka mitatu tayari kama ataweza kutua klabuni hapo na kusaidia kikosi hicho.
Tayari ana uzoefu ulioshiba ndani ya ligi hiyo kutokana na kuwa aliwahi kuwaongoza majirani wa klabu hiyo, Napoli na kwenda ndani ya Juve itakuwa ni nafasi yake nyingine kuonesha makali ambayo aliyaacha baada ya kwenda Uingereza lakini ndani ya klabu mpya na mabingwa wanaoheshimika.


Povel
Habar njema