Aliyekuwa menejja wa Juventus Massimiliano Allegri, amethibitisha kuwa anahitaji kupumzika soka kwa mda baada ya kuachana na majukumu ya umeneja pale Juve.
Allegri ambaye ana umri wa miaka 51 ameshinda jumla ya mataji matano ya Serie A akiwa na mabingwa wa ligi hiyo Juvetus kabla ya kuachia ngazi klabuni hapo.
Bwana Massimiliano Allegri alikuwa akihusishwa na klabu ya Chelsea wakati Sarri akienda kuchukua nafasi yake Juventus. Lakini meneja huyu amedai kwamba anahitaji kupumzika kwa mwaka mzima ili aweze kufanya mambo yake binafsi kwa uhuru zaidi bila kikwazo ili arejee kwa kasi nyingine.
“Ninaenda likizo ya mwaka mzima niweze kuzichaji betri zangu na kuweka sawa maisha yangu binafsi” –Allegri
Allegri alichaguliwa na Juventus mwaka 2014, wakati anaingia klabuni hapo mwanzoni kulikuwa na hali ya kutokukubalika na mashabiki. Lakini amewaachia zawadi ya mataji 4 ya Coppa Italia na kuwafikisha fainali ya ligi ya mabingwa mara 2.


Povel
Gud news
Zeiyana
Hatujui mwenyewe nini mawazo yake kwani ni kocha mwenyew uwezo mkubwa sana ni historia aliyo hacha kipindi yupo juventus hawawezi kuisahau unaweza ukasema kama ilikua zawadi ya mataji 4 ya coppa atalia na kuwakisha fainali ya ligi ya mabingwa Mara 2