Beki wa kushoto wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Uingereza Luke Shaw amefunguka na kusema kua timu hiyo ipo kwenye muelekeo mzuri, Lakini wanahitaji kufanya vizuri zaidi.

United ambao wapo chini ya mwalimu Eric Ten Haag ambae alianza vibaya klabuni hapo, Lakini kocha huyo amewafanya United kucheza mpira ambao unavutia kwasasa na kuanza  kurudi kwenye ule bora wao ambao wawatu wamekua wakiufahamushawMan United hawajapoteza michezo sita mpaka sasa tangu walipofungwa na Manchester City mwanzoni mwa Oktoba. Kutokana na hali ndio inamfanya beki wa klabu hiyo Luke Shaw kuona klabu ipo kwenye muelekeo mzuri ila wanahitajika kua bora zaidi.

“Nadhani kumekua na maboresho makubwa, Mwanzo wa msimu haukua vizuri kwetu na sote hilo tunalijua, Lakini nadhani toka wakati huo tumepiga hatua kubwa, Lakini tunahitaji kufanya vyema zaidi” Alisema beki huyo.shawBeki huyo pia alizungumza namna ambavyo kocha Ten Haag amebadilisha timu hiyo “Anazungumza na mchezaji mmoja mmoja sana nadhani, na hiyo amekua akifanya tangu wakati tunafanya maandalizi ya msimu mpya, Niliweza kujua ni aina gani ya meneja na nilivutiwa nae”Alisema Shaw

Beki huyo anaamini kocha huyo amebadili vitu vingi kwenye timu hiyo kwasababu ni mwalimu ambae anajua kuishi na wachezaji vizuri na kutaka kujua changamoto zao. Pia anahitaji wachezaji kujituma zaidi na zaidi.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa