Simba SC : Wachezaji Majeruhi Warejea, Kujiandaa dhidi ya Galaxy.

 

Kocha mkuu wa Simba SC, Didier Gomez amedhibitisha kurejea kwa wachezaji wake waliokuwa majeruhi kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana.

 

Wachezaji wa Simba SC, Kapombe na Kanoute walirejea na kuwa fiti na kuonesha kiwango safi kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Cambiasso huku kiungo Pape Sakho akiendelea kurejea taratibu na mazoezi ya kuweka sawa mwili.

Kocha huyo wa Simba SC, Gomes alidhibitisha: “Kanoute na Kapombe wako fiti na wanaendelea na programu za timu. Sakho anaendelea vizuri na nilipanga kumpa hata dakika 20 kwenye mechi ya leo (jana) dhidi ya Cambiasso kuona maendeleo yake licha ya kwamba nina uhakika Botswana atakuwepo.”

Sambamba na hayo pia Gomes amewazungumzia nyota wake waliokuwa katika timu zao za Taifa, Aishi Manula, Kibu Denis, Mohamed Hussein, Kennedy Juma, John Bocco (Tanzania), Peter Banda, Duncan Nyoni (Malawi), Rally Bwalya (Zambia), Meddie Kagere (Rwanda), Taddeo Lwanga (Uganda) na Joash Onyango (Kenya) huku akijivunia walichokifanya.

“Nilitazama mechi ya Taifa Stars walionesha kiwango bora, Manula alikuwa kwenye kiwango bora.” aliongeza Gomes.


PIGA MKWANJA NA LA ROUGE

Fanya wiki yako iwe ya kuvutia zaidi, tunaelekea Los Angeles kutengeneza mkwanja na kasino maridhawa ya LA Rouge kutoka katika kasino za mtandaoni za meridianbettz, Fursa ya kufurahi huku unajaza pochi yako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe