Simba Yachezeshwa Pira Gwaride

Wakiwa Uwanja wa Mkapa, mabingwa watetezi, Simba leo wamechezewa Pira Gwaride na kikosi cha Tanzania Prisons na kuwafanya wafanye msako mkali kutafuta bao la kufutia machozi kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Kipindi cha kwanza dakika ya 23, Chris Mugalu akiwa na kipa Jeremia Kisubi alipiga penalti iliyookolewa na kipa huyo wa Tanzania Prisons ambaye leo alikuwa kwenye ubora wake dakika zote 90 mpaka ubao ukasoma Simba 1-1 Tanzania Prisons.

Ni Salum Kimenya, kiraka wa Tanzania Prisons alianza kumtungua Aishi Manula dakika ya 56 kwa faulo aliyopiga nje kidogo ya 18 na ikapenya kwenye ukuta wa Simba na kumpoteza kipa namba moja Aishi Manula.

Baada ya bao hilo Didier Gomes alikuwa haamini anachokiona kwa kuwa vijana wa Prisons walikazana kucheza lile pira gwaride ambalo liliwafanya Simba wakazane kusaka ushindi huku mipango yao ikidhibitiwa.

Licha ya kwamba Prisons walikuwa 10 uwanjani baada ya Jumanne Elifadhil kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kumchezea faulo Mzamiru Yassin bado mambo yalikuwa mazito kwa Simba.

Mpaka dakika 90 zinakamilika ubao ulikuwa unasoma Simba 0-1 Prisons jambo lililowafanya Prisons waamini watasepa na pointi tatu nyingine kama walivyowatungua bao 1-0 Uwanja wa Nelson Mandela.

Katika dakika 5 za nyongeza zikiwa zinafika tamati, Luis Miquissone alimalizia pasi ya kichwa ya Bernar Morrison na kufanya ubao usome Simba 1-1 Prisons.

Sare hiyo inawafanya Simba wafikishe jumla ya pointi 46 wakiwa wamecheza mechi 20 huku wapinzani wao Yanga wakibaki kileleni na pointi zao 50 tofauti ya pointi 4.

Prisons wanafikisha jumla ya pointi 28 na wanapanda kutoka nafasi ya 10 mpaka ya 9.


Ni Burudani Iliyokithiri na Mkwanja Nje Nje Katika Mchezo Halisi wa Chicago Gold.

Fanikisha malengo yako bila kuumiza kichwa, tengeneza mkwanja bila wasiwasi na kasino ya Meridianbet. Jiunge sasa Ufurahie Chicago Gold kasino.

CHEZA HAPA

10 Komentara

    Simba nawakubali sana

    Jibu

    Simba wako vizuri

    Jibu

    Nacho wapendea simba awakubaligi kushindwa

    Jibu

    Wamekiona cha mtema kun

    Jibu

    Ha ha ha ha ha

    Jibu

    Walionewa sana

    Jibu

    Hadi jashoo liliwatokaa hahaha

    Jibu

    Simba kwa vizuri

    Jibu

    Simba kiboko yao

    Jibu

    Mikia mmepotea

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.