Klabu ya Singida Big Stars imepoteza mchezo wake wa kwanza hapo jana kwa bao 1-0 toka wapande ligi kuu ya NBC ambapo walikuwa ugenini kucheza dhidi ya Azam FC katika uwanja wa Chamazi jijini Dar es salaam.

 

Singida Big Stars Yapoteza Mchezo Wake wa Kwanza

Bao hilo lilifungwa na Sospeter Bajana baada ya kupiga kombora kali ambalo lilimuacha golikipa wa Singida United kuelea nyavuni na kufanya Azam wajipatie alama 3 muhimu ambazo mechi iliyopita walizipoteza.

Singida Big Stars imeweza kusajili wachezaji mbalimbali wenye uzoefu, akiwemo Pascal Wawa, Meddie Kagere, Metacha na wengine wengi ambao waliaminika watakuja kuisaidia timu hiyo ambayo inaonekana inaleta ushindani mkubwa kwenye NBC.

Singida Big Stars Yapoteza Mchezo Wake wa Kwanza

Baada ya kupoteza mchezo huo, timu hiyo inashikilia nafasi ya 5, huku ikiwa imecheza mechi 6 na alama zao 8 kibindoni.  Mechi ijayo ya ligi kuu atamualika Simba nyumbani kwake.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa